| Wakufunzi wanaoingia kufanya mtihani wa kupandishwa madaraja wakiwa katika picha ya pamoja wakisikiliza maelekeo kabla ya kuanza kufanya mtihani huo.Picha na Vero Ignatus Blog |
| Master Shihan Shalom Avitan 9th Dan akiwa anawapa maelekezo wakufunzi wanaofanya mtihani wa kupanda madaraja kabla ya darasa kuaza rasmi .Picha na Vero Ignatus Blog. |
Wapili
kushoto ni Afisa michezo wa Mkoa wa Arusha Mwamvita Okong'o ,walieko
kulia kwake ni Afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno,aliyepo
katikati ni muwakilishi kutoka kampuni ya Benson ,akifuatiwa na Master
Shihan Shalom Avitan na wa kwanza kulia ni Sensei Dady K.Ramadhan.Picha
na Vero Ignatus Blog.
Sensei
Taifa Liwawa akikabidhiwa cheti cha kuwa Master of Art wa 27 katika
shirikisho hilo ulimwenguni mwote .Picha na Vero Ignatus
Blog
Mmoja wa wakufunzi Ally Iddy akipokea cheti kwa
kufaulu kuingia Done ya tatu.Picha na Vero Ignatus Blog.
Na.Vero Ignatus ,Arusha.
Mafunzo ya
karate ya kimataifa yanayoambatana na kufanya mtihani wa kupanda madaraja
yamefanyika Jijini Arusha yakiongozwa na
Master Shihan Shalom Avitan, kutoka nchini Israel .
Mafunzo
hayo yamefunguliwa na Afisa michezo mkoa wa Arusha Mwamvita Okeng’o ambapo
amesema kuwa serikali imeipa michezo kipaumbele ili kupunguza tatizo la ajira
nchini na amewataka wanamichezo hao kuuambikiza katika jamii kwa
ujumla
Akijibu
risala iliyoandaliwa na West coast Shotokan internation Karate( ASS'N)
Afisa michezo huyo wa mkoa amesema kuwa serikali inafanya jitihada ili
kuwapatia eneo la kudumu la kufanyia mazowezi kama
walivyoomba.
Naye
afisa michezo wa Jiji la Arusha Benson Maneno amesema kuwa michezo
inaimarisha afya ,ni ajira hivyo ameitaka jamii kushiriki kikamilifu
huku
akiwasisitiza vijana kutumia fursa hiyo ili waweze
kujiajiri.
Muandaaji
wa mafunzo hayo hapa nchini Sensei Dady Ramadhan ambaye ni Mkufunzi kiongozi
amesema kuwa wapo wanakarate wanaocheza Shotokan ambao wana
daraja mbalimbali
katika taaluma hiyo miongoni mwao wapo waliofanya mtihani na wamepanda
daraja
Aidha
amesema kila mwaka wanamuita mwalimu na kufanya mitihani ,hivyo amewataka wale
wote wanaotaka kuifunza mchezo huo wahakikishe wanajicfunza kupitia wataalamu
ambao wamepitia mafunzo hayo na wenye uzoefu wa kutosha
“Unajua
kwa sasa mchezo huu unawaalimu wengi ambao wamevamia hawana taaluma kabisa
hivyo msikubali kuburuzwa na kufundishwa na hao watawapotosha na kuleta madhara
kwani hawazifahamu kanuni na miiko ya karate.”alisema sensei
Dady.
Kwa upande
wake sensei Taifa Liwewa ambaye ni Katibu wa shirikisho West Coast shotokan
Karate ambaye kitaaluma ni msanifu jukwaa(Stage Craft designer amesema kuwa
karate siyo mchezo wa kihuni wala wa watu wasio na elimu bali nimchezo wa watu
wote.
“kuna watu
wananishangaza sana wanadhania kuwa watu wote waliokuja kucheza karate ni watu
wasiokuwa na elimu,wahuni,siyo kweli mimi nimezaliwa nikaikuta karate nyumbani
kwetu,mama yangu mzazi ana miaka 70 lakini bado anacheza karate ,baba yangu
alikuwa naye anacheza ,kaka yangu vilevile ,mimi mwenyewe natamani watoto wangu
wacheze karate.”alisema sensei Taifa.
Amesema
kuwa karate ina sheria na taratibu zake ,ameongeza kuwa mchezo huo wenye
maadili,nidhamu,utiifu pamoja na uadilifu kwani unajenga mwili na kuimarisha
afya,amesema zipo nguzo 5za mazowezi,nguzo 9 za mafunzo, pamoja na
miiko ya karate 20.
Wakufunzi
walioshiriki katika kufanya mtihani idadi yao walikuwa 13 kutoka
Arusha,Kilimanjaro 1,Dar es salaam 4 na imeshirikisha vilabu
vitano,mafunzo hayo yalikuwa ya siku tatu kuanzia 18januari hadi 20
januari
Mafunzo
hayo yamefungwa rasmi na mwenyekiti wa chama cha karate mkoa wa Arusha
Sensei Dady K.Ramadhani,ambapo amesema kuwa mafunzo ya mwaka huu
yamekuwa mazuri na wanafunzi wamefanya mtihani kwa ufahaulu wa hali ya
juu,mafunzo kama haya yanatazamiwa kufanyika tena januari
2018
0 Comments