Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri Akiongea na watumisi wa Tume ya Mipango (hawapo pichani)
wakati wa mkutano wake na watumishi hao. Kulia ni Naibu Katibu Mtendaji
anayesimamia Klasta ya Sekta za Uzalishaji Bw. Maduka Kessy na wa kwanza
kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw. Abdulrahman
Mdimu akifuatiwa Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Biashara za Kimataifa na
Mahusiano ya Uchumi, Bw. Paul Sangawe.
Kaimu Katibu Mtendaji, Tume ya Mipango,
Bibi Florence Mwanri akiongea jambo na Naibu Katibu Mtendaji, Klasta ya Sekta za
Uzalishaji Bw. Maduka Kessy wakati wa mkutano na watumishi wa taasisi hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Ufuatiliaji, Bw. Omary Abdallah akitoa
taarifa fupi ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mipango katika kipindi cha
nusu mwaka, kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa
Rasilimali Watu Bw. Abdulrahman Mdimu akiwasilisha mada juu ya maadili kwa
watumishi wa umma katika mkutano uliowahusisha wafanyakazi wa Tume ya Mipango.
Mwanasheria wa Tume ya Mipango, Bibi
Nyanzala Nkinga akichangia jambo katika mkutano wa wafanyakazi wa Tume ya
Mipango.
Watumishi wa Tume ya Mipango wakifuatilia
kinachoendelea wakati wa mkutano uliofanyika katika ofisi za taasisi hiyo.
PICHA
ZOTE NA ADILI MHINA, TUME YA MIPANGO
....................................................................................
Na
Adili Mhina, DSM.
Katika kuitikia na
kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli la Serikali kuhamia Dodoma, Tume ya Mipango inatarajia kuanza
kuhamisha watumishi wake kuelekea Makau Makuu ya Nchi ifikapo mwezi Machi Mwaka
huu.
Taarifa hiyo imetolewa na Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alipokutana na
watumishi wa taasisi hiyo Ijumaa Januari 26, 2017 kwa lengo la kujadiliana
mambo mbalimbali yanayohusu taasisi hiyo.
Pamoja na agenda zingine
kujadiliwa katika kikao hicho, suala la kuhamia Dodoma lilionekana kuchukua nafasi
kubwa miongoni mwa wafanyakazi mara baada ya ratiba ya zoezi hilo kutolewa
rasmi ambapo wengi walionesha kufurahishwa na kutendo cha kutimiza ahadi ya
Rais kwa wananchi ya kuhamia Dodoma.
Mwanri alieleza kuwa Tume ya
mipango itahamisha watumishi wake katika awamu tatu ambapo makundi mawili
yanatarajiwa kuhamia Dodoma ndani ya mwaka huu.
“Kundi la kwanza kwa upande
wa Tume ya Mipango litaondoka mwezi Machi mwaka huu ambapo pamoja na mambo
mengine, watumishi wa kundi hili watakuwa na jukumu la kuandaa mazingira kwa
ajili ya kuwapokea watumishi wengine watakaohamia
baadae,” alisema Mwanri.
Aliongeza kuwa sehemu ya pili ya watumishi inatarajiwa kwenda Dodoma
kuanzia mwezi Septemba mwaka huu ambapo pamoja na watumishi wengine, kundi hilo
linajumuisha Mkuu wa Taasisi ambaye ni Katibu Mtendaji akiambatana na Wakuu wa
Klasta, Idara pamoja na Vitengo na kundi la mwisho linatarajiwa kuhama kuanzia
mwezi Machi, 2018.
Kikao hicho pia kilitoa fursa ya
kutolewa kwa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Tume ya Mipango katika
kipindi cha nusu mwaka, kuanzia Mwezi Julai hadi Disemba kwa mwaka wa fedha
2016/17.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mipango
na Ufuatiliaji, Bw. Omary Abdallah alieleza kuwa katika Kipindi hicho Tume ya
Mipango imefanikiwa kutekeleza majukum mbalimbali ikiwemo; kuandaa mapendekezo ya Mpango wa
Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2017/18 na kuendesha mafunzo kuhusu mwongozo wa usimamizi wa
Uwekezaji wa Umma katika ngazi ya
Sekretarieti za mikoa na mamlaka za
Serikali za mitaa nchini.
Mafanikio mengine ni kuendelea
kusambaza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa
Taifa wa Miaka Mitano (2016/17 – 2020/21) kwa wadau pamoja na kuendelea kuandaa mikakati minne ya utekelezaji wa Mpango wa Pili wa
Maendeleo wa Taifa unaendelea (Mkakati wa utekelezaji, Ugharamiaji, Mawasiliano na Ufuatliaji na Tathmini).
Aidha Tume ya Mipango ilifanikiwa kufuatilia utekelezaji wa
baadhi ya Miradi ya Maendeleo ya Kitaifa katika mikoa ya Mwanza, Dodoma,
Tabora, Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es salaam kwa lengo la kutathmini maendeleo
ya utekelezaji wa miradi na kuelewa changamoto zinazokabili utekelezaji wa miradi hiyo.
0 Comments