Jitihada za uokoaji zikiendelea Baadhi ya wafanyakazi wa Mgodi wa RZ wakishiriki kutoa vyuma kwenye eneo lililofukiwa
Mashine ya kutolea udongo uliojifukia ikiendelea na juhudi za kufukua ili kupata sehemu ya mlango wa kutokea.
Bomba za kupitisha Hewa ya OXJEN ikiwa imepitishwa chini kwa chini.
Mtambo unaopeleka hewa ukiangaliwa kwa makini.
......................................................................
IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
NI
SIKU ya pili sasa tangu wachimbaji kumi na nne (14) ambapo simanzi,
masikitiko yameendelea kutanda baina ya jamii na ndugu wa wachimbaji
ambao wamefukiwa na udogo kwenye Mgodi wa RZ uliopo Kijiji cha
Nyarugusu Wilaya ya Geita hata hivyo jitihada na zoezi la kuwaokoa bado
linaendelea .
Zoezi
la uokoaji linalosimamiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa, Ofisi
ya Madini Kanda ya ziwa magharibi ikiyashirikisha makampuni ya Migodi
ikiwemo GGM na Busolwa mine, imeelezwa hatua iliyofikiwa hadi leo saa
1:30 asubuhi walikuwa wamechimba takribani mita 20 kati ya 30 ili
kuwafikia wachimbaji hao.
Kufuatia
hatua hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga
aliwataka ndugu na jamaa wa watu 14 waliofukiwa na kifusi ndani ya
Mgodi wa RZ kuwa na subira wakati waokoaji wakiendelea na Zoezi hilo.
“Mimi
niwatake ndugu na jamaa kuendelea kuvuta subira wakati waokoaji
wakiendelea na kutumia mashine kwa ajili ya kuwaokoa watu waliozama
chini ya Mgodi huo jambo ambalo hata Mkoa wa Geita umelipokea kwa
masikitiko makubwa sana,’’alisema Kyunga.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa kalipio kali kwa wawekezaji ambao hawajali
ustawi wa wafanyakazi wake kwa uzembe ambao unaweza kuepukika na kwamba
alisikitishwa sana namna mgodi wa RZ ambavyo ulikuwa haujali masuala ya
miundombinu yake.
ZOEZI
la uokoaji limeendelea huku matumaini ya wengi yakizidi kupotea
kutokana na ugumu wa kazi dalili hata kidogo hazionekani lakini
kamishina wa madini kanda ya ziwa magharibi Bw. Yahaya Samamba amesema
zoezi hilo litakamilika na watu watakuwa salama kutokana na hewa
wanayoipata kupitia mpira unaoingiza kwa kutumia mashine.
Maduka
online usiku kucha imeshuhudia hatua kwa hatua zoezi hilo, licha ya
baadhi ya maafisa wa serikali wakishindwa kuvumilia kukesha kwenye zoezi
hilo.
Kamishina
msaidizi wa madini kanda ya Ziwa Yahaya Samamba ameendelea kuelezea
kuwa pamoja na kuunda kamati ya uokoji wamekutana na changamoto kubwa
kwa sababu ya duara walikozama watu hao kuwa chini ya kilomita 35.huku
akisema wanaendelea kuomba mashine nyingine kutoka kwa makampuni mengine
kama zoezi litaonekana kuwa na ugumu.
“Tumeunda
kamati ya uokoji na kamati yetu imehusisha makampuni yote yalioleta
mashine zao kwa ajili ya uokoaji huo huku naye akiwataka wananchi
kutoanza kutoa lawama kwa baadhi ya vyombo vya Serikali na ngazi
nyingine kwenye wizara ya madini,, alisema Samamba.
Maduka
online ilibahatika kukutana uso kwa uso na diwani wa kata ya Nyarugusu
yalipo maafa hayo, Swalehe Juma alisema janga hilo limemnyima usingizi
na kwamba siku ya jana alilazimika kukesha na waokoaji.
“Mwandishi
nakushukuru kwa kuwa nasi kwenye zoezi hili ni kweli mimi nyumbani ni
karibu hata kwa miguu naweza kutembea nikafika lakini siwezi kwenda
jambo hili limeninyima raha nitawezaje kwenda kwangu wananchi wangu wako
ndani ya shimo,’’alisema Juma.
Hata
hivyo baadhi ya wananchi waliohudhuria kushuhudia tukio hili la aina
yake katika wilaya ya Geita ikiwa ni mwanzoni mwa mwaka wa 2017,
walisema lawama kubwa wanazielekeza kwa mamlaka za madini kwa kushindwa
kujisimamia katika kuhakikisha uchimbaji ulio imara kwenye migodi
unaboreshwa.
“kaka
hili jambo linasikitisha sana hebu fikiria tangu usiku wa tarehe 26 saa
saba usiku mpaka leo siku nyingine ya tarehe 27 tumekutana tena watu
wako ndani ya kifusi je watapona licha ya matumaini tunayopewa…Mimi hapa
naelekeza lawama kwa ofisi ya Madini Mkoa wa Geita hawakagui migodi
ipasavyo,’’alisema Mkazi wa Nyarugusu Saidi Mrisho.
“Kwanza
nashangaa nilimsikia jana kamishina wa madini kanda ya ziwa akisema
chanzo ni kutokana na miti iliyokuwa imeshikilia ukuta kuwa imeoza sasa
hapa najiuliza je, kazi ya ofisi ya madini nini wanakagua nini na je
waliwahi kuwaambia kuwa miti hii haifai katika ukaguzi wao inapaswa
serikali nayo iwachukulie hatua kubwa kwa uzembe huu
haiwezekani,’’alisisitiza.
Katika
shughuli za uokoaji wananchi hawakuacha kuipongeza kampuni ya uchimbaji
wa madini ya Busolwa Mine inayomilikiwa na mwekezaji mzawa Baraka kwa
kujitolea mashine zake za greda kuhakikisha wanafanikisha adhima ya
kuwaokoa watanzania 13 pamoja na raia wa china Bw. Meng Juping, ambaye
anadaiwa hakuwa na redio koll kama ilivyokuwa kawaida yake wakati
anakwenda kutekeleza majukumu yake ya uzalishaji wa madini ya dhahabu.
Hata
hivyo Madukaonline ilishuhudia kikosi cha zima moto na uokoaji Mkoa wa
Geita pamoja na jeshi la polisi wakiendelea na majukumu yao ya
kuhakikisha eneo hilo liko salama.
0 Comments