Kaimu Muwakilishi Mkaazi wa UNFPA Tanzania Dkt. Hashina Begum na Waziri wa Afya
wa Zanzibar Mahmoud Thabit Kombo wakisaini makabidhiano ya magari manne ya
kubebea wagonjwa na mawwili ya huduma yaliyotolewa na Shirika hilo katika
sherehe zilizofanyika Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Dkt. Hashina akimkabidhi Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo moja ya funguo za
magari hayo kwenye sherehe zilizofanyika Wizarani kwake Mnazimmoja Mjini Zanzibar.
Gari nne za kubebea wagonjwa na mbili za huduma zilizotolewa msaada na Shirika
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Idadi ya Watu Ulimwenguni (UNFPA) kwa ajili ya kutoa huduma katika
Hospitali na vituo vya Afya Zanzibar zikiwa mbele ya Wizara hiyo Mnazimmoja
Mjini Zanzibar.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo akiwa na Kaimu Muwakilishi Mkaazi wa UNFPA
Dkt. Hashina Begum akilijaribu moja ya gari lilililotolewa msaada na UNFPA akwa
ajili ya kuhudumia wagonjwa.
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo na Kaimu Muwakilishi wa UNFPA Tanzania Dkt.
Hashina wakinyanyua moja ya vifaa tiba vilivyotolewa na UNFPA kwa ajili ya wodi
ya mama wajawazito na watoto.
Picha na
Makame Mshenga/Maelezo.





0 Comments