Magoli mawili ya kiungo mshambuliaji Raia wa Uingereza mwenye asili ya Algeria Dele Alli yametosha kuipunguza kasi Chelsea kwenye mbio za Ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Chelsea imepoteza mchezo wake
dhidi ya Tottenham Spurs baada ya kutandikwa jumla ya mabao 2-0 kwenye
uwamja wa White Hart Lane Mjini London alikuwa Dele Alli aliwanyanyua mashabiki wake dakika ya 45 akifunga bao la utangulizi kwa wenyeji hadi mapumziko Spurs walikuwa mbele.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila
timu kufanya mabadiliko huku Chelsea wakiingia na kasi ya kutaka
kusawazisha hata hivyo juhudi zao zilizimwa dakika ya 54 Dele Alli alifunga bao la pili kwa Spurs.
Baada ya kupigwa bao la pili
Chelsea walipanic na kuanza kucheza Mpira wa nguvu na ubabe hadi mwamuzi
anamaliza Mpira Spurs wameibuka na ushindi wa jumla ya magoli 2-0.
Na Matokeo hayo yameifanya Spurs
kuchupa hadi nafasi ya tatu wakiwa na pointi 42 huku wapinzani wao
wakubwa wa jiji la London Arsenal wakishuka hadi nafasi ya tano wakiwa
na pointi 41 wakati Chelsea wamebaki kwenye kilele mwa Ligi wakiwa na
pointi 49 huku wakiwa wanawazidi Liverpool pointi tano kwani wana alama
44.
|
0 Comments