Mtaalamu wa lishe katika
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Mariam Nyamwaira akizungumza na
waandishi wa habari leo kuhusu maadhimisho ya wiki ya lishe ambayo yameanza leo Januari 30, 2017 na yatahitimishwa Februari 03, mwaka huu.
Kulia ni Mtaalamu wa Lishe, Elizabeth Lyimo wa hospitali hiyo.
Waandishi wa habari
wakimsikiliza mtaalamu huyo wakati akiwaeleza lengo la maadhimisho ya wiki ya
lishe ambayo yanafanyika kwenye hospitali hiyo katika Jengo la Wagonjwa wa Nje
(OPD).
Baadhi ya watu waliopima afya
wakipatiwa ushauri kutoka kwa wataalamu Mariamu Nyamwaira (kushoto) na Elizabeth Lyimo (kulia).
................................................................................
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
inaadhimisha wiki ya lishe kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa
kuzingatia lishe bora ikiwamo kupima wingi wa mafuta mwilini.
Maadhimisho hayo yana lenga
kupunguza magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, magonjwa ya moyo,
magonjwa ya figo na saratani.
Mtaalam wa lishe kutoka katika
hospitali hiyo, Mariam Nyamwaira amesema
katika maadhimisho hayo, wataalamu
wa lishe watapata fursa ya kutoa ushauri kuhusu suala la lishe, uhusiano wa
lishe na mazoezi, kupima urefu na uzito pamoja na kupima wingi wa mafuta
mwilini .
"Lengo ni kuweka uelewa wa suala
la lishe kwani ulaji usiofaa unachangia kwa kiasi kikubwa watu kupata magonjwa
yasiyoambukiza hivyo kupitia wiki hii tunatoa huduma bure na endapo mtu
akibainika kwamba katika hali hatarishi tutamuingiza kwenye kliniki zetu ambazo zinafanyika hapahapa Muhimbili ,"amesema
Bi Nyamwaira.
Leo jumla ya watu 78 wamepimwa wingi
wa mafuta mwilini na kupewa ushauri wa lishe bora na kati ya hao asilimia 85
wapo hatarini kupata magonjwa yasioambukiza kutokana na kuzidi uzito.
Maadhimisho hayo yameanza Januari 30,
2017 na yatahitimishwa Februari 03, 2017.



0 Comments