MKuu wa Mkoa AELEKEZA safari za kikazi kwa
watumishi wa serikali Mkoa wa Mbeya
kutumia shirika la Ndege la Taifa(ATCL)
Asema Uwanja
wa Ndege wa kimataifa wa Songwe Ukikamilika utakuwa ni lango
la kuingia Tanzania kwa nchi zote za kusini mwa Afrika
Ameiomba
ATCL watakapoingiza Ndege nyingine
kuweka katika Mipango ya safari za Mbeya - Malawi- Dar
Uongozi wa shirika
la Ndege la Taifa( Air Tanzania) umehaidi kuendelea kutoa huduma bora kwa
wateja wake nchini kote ikiwa ni sehemu
YA mikakati yake YA kibiashara
Hayo yamesemwa
leo na mwenyekiti wa bodi YA ATCL Ndg Emanuel Koroso na Mtendaji Mkuu wa ATCL
Eng Ladislaus Matindi walipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla
Wamewashukuru sana
wananchi wa Mkoa wa Mbeya na watanzania wote kwa ujumla kwa ushirikiano
wanawapa wa kutumia shirika hilo ktk Safari zao na wamewaomba kuendelea
kulitumia shirika hilo ambalo limeboresha huduma zake
Mkuu wa Mkoa
amelishukuru shirika la Ndege kwa kuweka Mkoa wa Mbeya ktk Safari zake na
kufanya hivyo limepunguza kero ya wananchi kukwama kusafiri kama ilivyokuwa
hapo awali
Aidha ameliomba
shirika hilo kuweka ktk Mipango yake watakapopata Ndege zingine kutoa huduma
kwa nchi za jirani ikiwemo Malawi na zambia kwa kupitia uwanja wa Ndege wa
songwe.
No comments:
Post a Comment