Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, Eng. Kapuulya
Musomba akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Mradi wa LNG.
Kaimu
Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC, Eng. Kapuulya
Musomba (Kulia) , kushoto, Mkurugenzi wa usafirishaji na usambazji wa gesi
asilia, Dk. Wellngton Hudson .
Waandishi wa habari wakiwa katika mkutano huo.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON-FULLSHANGWEBLOG
Shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu mradi wa kusindika gesi asilia kimiminika (LNG), kufuatia taarifa zilizochapishwa kwenye gazeti la the Guardian la Tarehe 13 Februari, 2017, yenye kichwa cha habari “Tanzania LNG Project Stalls as Uncertainty rises-report”. Tafsiri ya kichwa cha habari inaonesha kwamba mradi umesimama, ama hatma yake haijulikani. Kichwa hiki cha habari hakina usahihi kwa kuwa mradi unaendelea vema, hatua mbalimbali za utekelezaji zimefikiwa na mipango ya utekelezaji inafahamika.
TPDC kama mbia katika mradi huu inapenda kutoa ufafanuzi na kueleza hatua mbalimbali za mradi zilizofikiwa hadi sasa.
HATUA ZILIZOFIKIWA HADI SASA
1. Ardhi kwa ajili ya ujenzi wa awali wa mradi imeshapatikana katika eneo la Likong’o Mkoani Lindi na tayari Wizara ya Ardhi imeshatoa hati ya umiliki (title deed).
2. Takwimu mbalimbali zinaendelea kukusanywa baharini na nchi kavu aidha stadi mbalimbali za awali zinaendelea kubaini namba bora ya ujenzi wa mabomba na mitambo.
3. Upembuzi yakinifu wa kihandisi kuhusu uzalishaji na usafirishaji wa gesi hadi nchi kavu umefikia hatua ya kuridhisha. Gesi itasafirishwa kwa mabomba kutoka baharini hadi nchi kavu kwa umbali wa kilometa 80 hadi 200. Gesi itakayotumika katika mradi huu imeshagunduliwa kwenye vitalu namba 1, 2 na 4.
4. Majadiliano ya makubaliano ya namna ya uendelezaji wa mradi baina ya Serikali na Makampuni ya Mafuta ya Kimataifa yaliyowekeza katika mkondo wa juu (IOCs) yanaendelea vema.
HITIMISHO
1. Hatua za utekelezaji wa mradi zinafahamika
2. Takwimu zinazohitajika kwa ajili ya mradi zinazohitajika kwa ajili ya mradi zinaendelea kukusanywa
3. Stadi mbalimbali za kubaini utekelezaji bora wa mradi zinaendelea
4. Majadiliano baina ya serikali na makampuni ya mafuta ya kimataifa yanaendelea.
Hivyo basi dhana ya kuona kama hatma ya mradi haijulikani sio sahihi.
TPDC kwa maendeleo ya Taifa.
Imetolewa na
Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania

0 Comments