Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa DAWASA
Mhandisi Romanus Mwangi’ngo akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu mikakati ya
Serikali kuhakikisha kuwa changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam inapatiwa ufumbuzi wa kudumu mara baada ya kukamilika kwa miradi ya Ruvu Juu na Chini
pamoja na ule wa uchimbaji wa Visima Virefu katika eneo la Kimbiji vitakavyozalisha maji yatakayotumika katika
Jiji la Dar es salaam na Viunga vyake likiwemo eneo la Kigamboni.
Moja ya mitambo inayotumika kuchimba visima
katika eneo la Kimbiji ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano
kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam na
Viunga vyake.
Moja ya Kisima kilichochimbwa katika eneo la
Kimbiji kama kinavyoonekana,Kisima hicho
ni moja ya visima vinavyochimbwa katika eneo hilo hali itakayochochea maendeleo
katika Wilaya ya Kigamboni,Temeke na jiji la Dar es salaam kwa ujumla mara
baada ya kukamilika kwa mradi huo na
ujenzi miundombinu ya kusafirishia maji hayo.
Sehemu ya Kisima kama inavyoonekana katika Picha
Maji yakitoka kwenye moja ya Kisima Kirefu
kilichochimbwa katika eneo la Kimbiji unakotekelezwa mradi mkubwa wa unaolenga
kutatua changamoto ya maji katika Jiji la Dar es salaam.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika eneo
la Kimbiji wakati wa ziara ya kutembelea moja ya miradi mikubwa ya uchimbaji Visima Virefu inayotekelezwa na Serikali katika kutatua
chanagamoto ya upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam.
Moja ya Mitambo inayotumika katika uchimbaji wa
Visima Virefu katika eneo la Kimbiji,mradi huo ni moja ya mikakati ya Serikali
katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji katika jiji la Dar es salaam.
Mtambo unaotumika katika uchimbaji Visima Virefu
ukiwa katika eneo la mradi huo.
Sehemu mojawapo
vinapochimbwa Visima virefu vitakavyosaidia kuondoa chanagamoto ya
upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam.
Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa DAWASA
Mhandisi Romanus Mwangi’ngo akiwaongoza
kuelekea katika moja ya maeneo ya utekelezaji wa mradi huo. wataalamu wa
Kampuni ya Serengeti Ltd na ile ya NSPT ya Iran zinazotekeleza mradi wa
uchimbaji Visima Virefu katika eneo la Kimbiji
Msimamizi wa mradi wa uchimbaji Visima Virefu kutoka
wa Kampuni ya Serengeti Ltd Bw. Peter Flahant
akionesha kwa waandishi moja ya mitambo katika eneo la kimbiji na jinsi
inavyofanya kazi katika uchimbaji wa visima Virefu.
Msimamizi wa mradi huo toka kampuni ya Serengeti
Ltd Bw.Peter Flahant (katikati) akimsikiliza Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji
wa DAWASA Mhandisi Romanus Mwangingo.(kushoto) kulia ni mshauri wa mradi huo
Bw. Roland Chombo.
Msimamizi wa mradi huo toka Kampuni ya Serengeti Ltd Bw.MehrdadTalik
(katikati) akisitiza Jambo kwa Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa DAWASA
Mhandisi Romanus Mwangingo.(kushoto) wakati wa ziara ya waandishi wa habari
kutembelea mradi wa uchimbaji Visima virefu katika eneo la Kimbiji kulia ni
mshauri wa mradi huo Bw. Roland Chombo.
Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa DAWASA
Mhandisi Romanus Mwangingo akionesha kwa waandishi wa habari hawapo (pichani)
eneo unapotekelezwa mradi mkubwa wa uchimbaji Visima Virefu viyakavyozalisha
maji yatakayotumika katika Jiji la Dar es salaam.
Mshauri wa mradi huo Bw. Roland Chombo akisisitiza
Jambo kwa Mkurugenzi wa Ufundi na Uendeshaji wa DAWASA Mhandisi Romanus Mwangi’ngo.kulia
ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Serengeti Ltd Bw.Mehrdad Talik.
Moja ya Mitambo inayotumika katika uchimbaji wa
Visima virefu ukiwa katika eneo la mradi.
Sehemu ya Mitambo inayotumika kuchimba Visima
Virefu.
Mtambo unaotumika kuchoronga Visima Virefu ukiwa
katika eneo la Kimbiji unapotekelezwa mradi mkubwa wa uchimbaji visima virefu.
Tanki linalotumika kuhifadhi maji katika miradi
iliyobuniwa na DAWASA katika eneo la mbagala na kuendeshwa na wananchi wenyewe
ikiwa ni mkakati wa Mamlaka hiyo kuibua miradi ili kuondoa changamoto ya
upatikanaji wa maji katika Jiji la Dar es salaam.
Meneja Uhusiano wa DAWASA Bi Neli Msuya akieleza
kwa waandishi wa habari faida za miradi inayoibuliwa na Mamlaka hiyo kwa
kushirikiana na wananchi katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji
katika Jiji la Dar es salaam.
(Picha zote na Frank Mvungi-Maelezo)
Frank Mvungi-Maelezo.
...................................................
Serikali kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
Dar es Salaam (DAWASA) inatekeleza mradi
wenye thamani ya bilioni 18 unaolenga kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji
katika Jiji la Dar es Salaam.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa ufundi
na uendeshaji wa Mamlaka hiyo Bw. Romanus Mwang’ingo wakati wa ziara ya
waandishi wa habari katika eneo la Kimbiji ambako ndipo mradi huo unapotekelezwa
.
“Mkandarasi anaendelea na kazi na ameleta mabomba yote na amechimba visima 15
na vitazalisha maji yatakayotumika katika Jiji la Dar es salaam na mradi
unatarajiwa kukamilika machi 2017” Alisisistiza Mwang’ingo.
Aliongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo umefikia
asilimia 85 na utakapokamilika maeneo ya Kigamboni,Temeke,Ilala na Jiji la Dar
es Salaam kwa ujumla yatanufaika kwa kupata huduma ya maji.
Kwa upande wa miradi mingine kama ule wa ujenzi wa bomba kutoka
Ruvu juu hadi kimara Mwang’ingo amesema ulikamilika mwezi oktoba 2016 na uzalishaji wa
majaribio unaendelea
Mradi huo wenye thamani ya dola za marekani milioni 59 ni moja ya mikakati ya Serikali
katika kuhakikisha kuwa wakazi wa Jiji la Dar es salaam wanapata huduma ya maji
safi na salama. na kuondokana na changamoto hiyo. .
Aidha mradi huo utawezesha kiwango cha maji
kufikia lita milioni 196 kwa siku kutoka lita milioni 82 za awali.
Kwa upande wake Bw.Salum Hamis mkazi wa mbagala amepongeza miradi ya
maji inayotekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi kwa kuwa imekuwa chachu
ya maendeleo katika maeneo yao.
Aliongeza kuwa miradi hiyo imechochea kupunguza tatizo la maji na imewawezesha wananchi kutumia muda mwingi
katika shughuli za kiuchumi na hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi.
Katika kukabilina na tatizo la miundombinu ya maji
taka katika Jiji la Dar es Salaam mamlaka hiyo iko katika mchakato wa kuanza
ujenzi wa mtambo mkubwa wa kuchuja maji taka katika eneo la Jangwani na kuboresha mfumo wa maji taka katikati ya
Jiji.
Mradi mwingine ni ule wa upanuzi wa ruvu chini ambao
umekamilika kwa asilimia mia moja na utawezesha upatikanaji wa maji kufikia
lita milioni 270 kwa siku kutoka milioni 180 kabla ya mradi huo haujatekelezwa.
Majukumu ya DAWASA
ni kumiliki miundombinu ya maji safi na maji taka kwa niaba ya Serikali,
kusimamia utoaji wa huduma ya maji safi na maji taka Dar es salaam, kugharimia,kupanga
mipango na kusimamia upanuzi wa huduma na kuishauri Serikali kuhusu masuala ya
huduma ya maji safi na maji taka Jijini
Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment