Na:
Lilian Lundo – MAELEZO - Dodoma
Bunge
la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania leo, Mjini Dodoma limepitisha muswada wa
sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali (Na. 4) wa mwaka 2016 [The written
laws miscellaneous Amendments (No. 4) Bill, 2016].
Akiwasilishwa
muswada huo Bungeni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa
muswada huo unapendekeza kufanya marekebisho katika Sheria Sita ambapo lengo la
marekebisho yanayopendekezwa ni kurahisisha utekelezaji wa Sheria hizo kwa
kuondoa upungufu uliojitokeza wakati wa kutumia masharti ya sheria hizo.
Masaju
alizitaja sheria zilizopendekezwa kufanyiwa marekebisho kupitia muswada huo
kuwa ni Sheria ya Mikopo, Misaada na Dhamana, Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu
ya Juu, Sheria ya Kodi ya Mapato, Sheria ya Ardhi, Sheria ya Sukari na Sheria ya Hifadhi ya Wanyamapori.
“Ibara
ya 21 ya muswada inapendekeza marekebisho katika kifungu cha 30 cha Sheria ambacho
kinaweka masharti kuhusu Waziri mwenye dhamana ya fedha kukasimu madaraka yake
chini ya Sheria hiyo. Sheria ilivyo sasa inaelekeza kuwa Waziri anaweza
kukasimu mamlaka yake ya kujadili mkopo (negotiating loan), kuingia makubaliano
ya kukopa mkopo na kutoa dhamana,” alifafanua Masaju.
Aliendelea
kwa kusema kuwa muswada unapendekeza kuwa Waziri awe na uwezo wa kukasimu pia
mamlaka ya kujadili au kuingia makubaliano ya misaada kwa mamlaka au mtu
mwingine. Lengo la marekebisho hayo ni kurahisisha taratibu za upokeaji misaada
kwa kuwa sheria hiyo ilikuwa kimya kuhusu suala hilo.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la Katiba na Sheria,
Mohamed Mchengerwa alipokuwa akitoa maoni na ushauri wa kamati hiyo alisema
kuwa, kamati hiyo inaunga mkono marekebisho ya Sheria ya Mkopo wa Elimu ya Juu kwa
sababu itatoa nafasi kwa Watanzania wengi wa kipato cha chini kupata nafasi ya
kusoma katika Vyuo vya Elimu ya Juu.

Aidha
ameeleza kuwa, kamati inakubaliana na mtazamo wa Serikali kwamba utoaji wa
Mikopo ya Elimu ya Juu kwa ajili ya ngazi ya Diploma utazingatia vipaumbele vya
Taifa kulingana na wakati husika.
Nae,
Mbunge wa Karagwe, Innocent Bashungwa
amesema kuwa muswada huo umelenga kusaidia Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupata mikopo yenye
riba nafuu.
Vile
vile muswada huo unapendekeza marekebisho katika sheria ya Wanyamapori kuwa,
katika hatua yoyote ya kesi ya Mahakama inaweza kwa kuamua yenyewe au kwa
maombi ya upande wa mashtaka kutoa amri
kuwa mnyama, nyara ya Serikali, silaha, gari au kitu chochote kilichotolewa
kama ushahidi ambacho kinaweza kuharibika au kupoteza thamani kiuzwe au
kiharibiwe na Mkurugenzi wa Wanyamapori.
Pia
muswada huo unapendekeza kuongezwa kifungu kipya kitakachoweka masharti kuhusu
bei elekezi ya miwa, sukari na bidhaa nyingine zitokanazo na miwa.
Mwenyekiti,
Mhe. Najma Giga alitangaza rasmi kupitishwa kwa muswada huo na Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania baada ya kupata kura nyingi za ndio. Aidha muswada huo
unasubiri kibali cha Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili uanze kutumika kama
sheria.

0 Comments