Mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan
(kulia), akipokea cheti cha utambulisho wa kuwa balozi wa Amani kutoka kwa Mkurugenzi
Mkazi Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi.
Mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan
(kulia), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuteuliwa kuwa balozi
wa amani Tanzania. Kushoto ni Mkurugenzi Mkazi Taasisi ya Global Peace
Foundation (GPF) Martha Nghambi.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Global Peace Foundation
(GPF) Tanzania, Martha Nghambi (wa pili kushoto) na mshindi wa Big Brother Africa
Hotshots 2014) Idris Sultan (wa tatu kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kutangazwa kuwa balozi wa amani kwa vijana Tanzania.
..........................................................................
Na Mwandishi wetu
Taasisi ya Global Peace Foundation (GPF) Tanzania, imemteua
mshindi wa Big Brother Africa Hotshots 2014) Idris Sultan, kuwa balozi wa amani
kwa vijana duniani.
Mkurugenzi Mkazi wa GPF Tanzania, Martha Nghambi alisema
kuwa wameamua kumtumia Idris kutokana na mvuto wake kwa vijana na kutokana na
hilo atafikisha ujumbe kirahisi kwa vijana ambao ni zaidi ya asilimia 60 ya
idadi ya watu Tanzania.
Alisema kuwa bado kuna changanoto nyingi za kudumisha amani
duniani kwani mpaka sasa kuna baadhi ya nchi zipo katika matatizo makubwa
yaliyosababishwa na uvunjifu wa amani.
Martha alisema kuwa Idris ni mtu sahihi katika kampeni yao
na wanaamini kuwa kupitia yeye vijana na watu wengine watapata ujumbe wa
kuhamaisha kudumisha amani duniani.
“Kuna baadhi ya nchi zina
matatizo ya amani, waswahili wanasema, ukiona kwa mwenzako kunawaka moto… kwako
andaa maji, sisi tumeamua kuchukua tahadhari mapema ili kulinda amani yetu,”
Kwa upande wake, Idris alifurahi sana kupewa nafasi hiyo
ambayo ni kubwa sana katika maisha yake.
“Wamenithamini na kuniona ninafaa katika kampeni hii, ni
kweli, amani inatakiwa kuanzia kwenye familia mpaka juu ambako wengi wanadhani
vita tu ndiyo inatakiwa kupigiwa kelele, vijana ndiyo nguvu kazi ya ya taifa na hivyo
tunatakiwa kuwa na mawazo yaliyopanuka ili kujipatia vipato na kuachana na
lawama kutokana na kukosa soko la ajira,” alisema Idris.
Alifafanua kuwa kuwa balozi ni jukumu zito na atalitumikia
ipasayo ili kufikia malengo yaliyowekwa. “Amani ni kazi ya kila siku na ni muhimu, leo hii
wasanii wanaigiza na wanamuziki wanafanya kazi zao bila kuwa na woga, hii yote
inatokana na amani,” alisema.
Global Peace Foundation ni shirika lisilo la kiserikali na lisilo tengeneza faida lenye makao yake
makuu, mjini Washington DC, Marekani. Shughuli kubwa la shirika hili ni kuhamasisha
amani duniani kupitia matawi yake mbalimbali duniani.
Mbali ya Tanzania, matawi mengine katika bara la Afrika ni
Kenya, Uganda na Nigeria. Kauli mbiu ya shirika hilo ni “We are all “One
family under God” (sisi wote ni familia moja kwa Mungu).
Kwa sasa Global Peace Tanzania inaendesha kampeni ya
kuhamsisha amani kuanzia ngazi ya familia ijulikanyo kama “Vijana na Amani”.
Kupitia kampeni hii, GPF Tanzania inahamasisha amani kwa kutoa elimu katika
shule, vyuo na jamii kwa ujumla.




0 Comments