Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza
wakati wa mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Ofisini
kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya tathimini ya
utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara katika
Halmashauri nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita
Kapteni Mstaafu John Chiligati.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu
John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao baina ya kamati hiyo na TAMISEMI
kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri mbalimbali
nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe na Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe
akifafanua jambo wakati wa kikao baina ya Kamati ya Uongozi ya MKURABITA na
TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo katika Halmashauri
mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George
Boniphace Simbachawene, Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa
Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania (MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John
Chiligati na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo
Lupala.
Watendaji kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ambao ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Miji Dkt.
Mkuki Hante pamoja na Mkurugenzi wa Utawala kwa Serikali za Mitaa Bibi. Miriam
Mmbaga wakifuatilia mjadala wakati wa kikao baina ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais – TAMISEMI na MKURABITA kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo leo
Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akipokea
taarifa ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha rasilimali na
biashara uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9 nchini kutoka kwa Mwenyekiti
wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati leo Jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akisoma taarifa
ya tathmini kuhusu utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha rasilimali na biashara
uliofanyika katika Halmashauri 52 na Miji 9 nchini mara baada ya kuipokea kutoka
kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati(hayupo
pichani) leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace
Simbachawene akiteta jambo na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita
Kapteni Mstaafu John Chiligati (katikati) Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi
wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala mara baada ya
mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya hiyo Ofisini kwake leo Jijini
Dar es Salaam.
Na: Mpiga Picha Wetu.
..........................................................
Na: Frank Shija –
MAELEZO.
27/02/2017
Kufuatia kusuasua kwa
utekelezaji na maendeleo ya Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara
Serikali imeziagiza Halmashauri zote nchini ambazo zimefikia na mpango huo
kuwasilisha taarifa rasmi.
Agizo hilo limetolewa
na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.
George Boniphace Simbachawene katika kikao baina yake na wajumbe wa Kamati ya
Uongozi wa MKURABITA kilichofanyika Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam.
Simbachawene amesema
kuwa TAMISEMI ni mdau muhimu katika Mpango huo wa urasimishaji wa rasilimali
hivyo ujio wa kamati hiyo kutaka kushirikiana na Tawala za Mikoa ni jambo jema.
“Binafsi ni muumini
wa muda mrefu wa mpango huu wa urasimishaji, niseme tu mmechelewa kuja sehemu
husika kwa bila dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi kufanikiwa kwa
mpango huu itakuwa ni adithi sasa tutaenda pamoja ili kiutimiza azma ya mpango
huu,”alisema Simbachawene.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Kapteni wa Jeshi Mstaafu John
Chiligati amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa Halmashauri zaidi ya 100 nchini
mpaka sasa utekelezaji wa mpango huo umezifikia takribani Halmashauri 52 na
Miji 9 tu hivyo kasi yake bado hairidhishi.
Aliongeza kuwa
changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa mpango huo ni Halmashauri
kuuona mpango huo kama hawahusiki nao hali inayopelekea kushindwa kuendelea
pindi mwakilishi wa Mkurabita atakapo ondoka katika eneo husika.
Chiligati amesema
kuwa baada ya kubaini changamoto hiyo waliamua kuwa na makubaliano maalum na
TAMISEMI juu ya utekelezaji wa pamoja wa mpango huo jambo ambalo wanaendelea
kulifanyia kazi.







0 Comments