Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira, akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara yake wa Fungu 51 kuhusu masuala mbalimbali ya kiutendaji. Kikao hicho ambacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka kimeandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), (hawapo pichani). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Simba Yahya na Mwenyekiti wa chama hicho, William Mkombozi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Simba Yahya,
akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara yake wa Fungu 51 kuhusu masuala mbalimbali
ya kiutendaji. Kikao hicho ambacho kinafanyika mara mbili kwa mwaka
kimeandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), (hawapo
pichani). Mkutano huo ulifanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira.
Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti
wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali
Kuu na Afya (TUGHE), Tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi
akizungumza na Wafanyakazi wenzake wa tawi hilo (hawapo pichani), wakati wa
mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es Salaam. Katikati
ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu
Mkuu, Balozi Simba Yahya.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkurugenzi
wa Utawala na Rasilimali Watu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Lilian Mapfa
akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa kwenye idara yake wakati wa mkutano wa Wajumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa
Serikali Kuu na Afya (TUGHE), katika mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara
hiyo, jijini Dar es Salaam.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nch.
Mjumbe wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwanaidi Shabaani akiuliza swali kwa Katibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (hayupo pichani), wakati wa mkutano uliofanyika Makao Makuu ya Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO
SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI





0 Comments