Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipokea risala toka kwa Kaimu Mkuu wa
Magereza Mkoa wa Tabora Mkuu wa gereza SSP Nahman Koko wakati yeye na
mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya
mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa mahabusu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi zawadi Naibu Mkuu wa
gereza la Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi wakati
yeye na mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza
ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na
mahabusu leo Februari 14, 2017.
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa zawadi Naibu Mkuu wa gereza la
Mahabusu Tabora Mrakibu wa Magereza Godliver Makwaruzi wakati yeye na
mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya
mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu
leo Februari 14, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wakitoka katika gereza la wanawake Tabora walipotembelea
Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa
na mahabusu leo Februari 14, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri
akiwashukuru sana kutembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa
zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli akiongea wakati yeye na Mke wa Waziri
Mkuu Mama Mary Majaliwa walipotembelea Magereza ya mahabusu ya Tabora
na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu leo Februari 14,
2017
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wakitoa zawadi kwa ajili ya wafungwa na mahabusu walipotembelea
Magereza ya mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa
na mahabusu leo Februari 14, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wakiagana na askari magereza bada ya kutembelea Magereza ya
mahabusu ya Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa wafungwa na mahabusu
leo Februari 14, 2017
PICHA NA IKULU
............................................................................
NA
MWANDISHI MAALUM
MKE
wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli pamoja na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wametembelea Gereza la Mahabusu Tabora na kutoa zawadi mbalimbali kwa
wafungwa na mahabusu gerezani hapo.
Wake
wa viongozi wametembelea gereza hilo leo (Jumanne, Februari 14, 2017) wakiwa katika ziara mkoani Tabora, ambapo Mama Janeth amesema
wameamua kuwatembelea wafungwa na mahabusu hao kwa nia ya kuwafariji kwa kuwa
wao ni sehemu ya jamii.
“Vitabu
vitakatifu vinasema kwamba ukiwasaidia watu wenye mahitaji utakuwa umetoa
sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu, hivyo tumeamua kuja kutembea wafungwa na mahabusi kwenye gereza hili na
kuwapa zawadi kwa kuwa nanyi mnahitaji faraja,” amesema.
Amesema
wameamua kwenda kuwaona wafungwa na mahabusu hao kwa lengo la kuwafariji na kuwatia
moyo kwa sababu wanaimani kwamba wakitoka watakuwa raia wema na hayo
wanayopitia ni sehemu ya kufanya marekebisho ya tabia.
“Ni
siku kubwa kwangu, nimejifunza mengi baada ya kufika hapa. Kitendo cha kwenda kuwaona
wenye mahitaji wakiwemo wagonjwa, wafungwa ni jambo jema tunaamini hizi zawadi
tulizozitoa zitawasaidia kwa sababu tunajua mnamahitaji mengi,” amesema.
Katika gereza
hilo wake hao wa viongozi wamekabidhi zawadi mbalimbali kwa wafungwa na
mahabusu, ambapo mwakilishi wa wafungwa hao Deo Kitave aliwashukuru kwa niaba
ya wenzake. “Tunawashukuru kwa kutukumbuka, tunamuomba Mwenyezi Mungu muendelee
kuwa na moyo huo,”.
No comments:
Post a Comment