Madaktari Bingwa
wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge
(kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa kifaa
kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa
kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia
wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu
ya moyo ya bila kufungua kifua (Catheterization).
Madaktari Bingwa
wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge
(kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa betri
ambalo litatumiwa na kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la
kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo
wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma mbalimbali za matibabu ya moyo ya bila
kufungua kifua (Catheterization).
Daktari bingwa wa Moyo wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuhudumia
Monica Mahenge ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo baada ya kufanyiwa matibabu
ya moyo kupitia mishipa ya damu bila
kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab . Monica ni
mmoja kati ya wagonjwa 16 ambao JKCI kwa kushirikiana na wataalamu kutoka
Hospitali ya BLK ya nchini India walitoa huduma za matibabu ya kuzibua milango
ya moyo (Valve), balloon mitral valve procedure
(Valvuloplasty), kuzibua mishipa ya damu ya moyo, kufunga kifaa kitakachosaidia moyo kupata
umeme (Pacemaker) na kuangalia utendaji kazi wa Moyo.
Madaktari bingwa
wa Moyo, Wauguzi, Technologists,
wataalam wa dawa za usingizi wakiwa
katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kumpatia mgonjwa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo
(Valve) bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab .
Kazi ya kutoa huduma ya matibabu
ya Moyo kwa mgonjwa kupitia mishipa ya damu bila kufungua kifua (Catheterization) kwa
kutumia mtambo wa Cath lab ikiendelea.
Picha na Anna Nkinda –
JKCI
No comments:
Post a Comment