Kesho Alhamisi Februari 16, 2017
timu za mpira wa miguu za Simba na African Lyon zitacheza mechi yao
katika Raundi ya Sita ya kuwania Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
yaani Azam Sports Federation Cup.
Mchezo huo awali ulipangwa kufanyika Machi mosi, 2017 lakini ulirudishwa nyuma kwa sababu za kiufundi kutoka timu zote mbili.
Michuano ya raundi hiyo ya sita,
itaendelea tena Februari 24, mwaka huu kwa michezo minne kuchezwa kwa
siku hiyo kuanzia saa 10.00 jioni kasoro mchezo mmoja tu utakaochezwa
saa 1.00 jioni.
Michezo ya siku hiyo kwa mujibu
wa ratiba inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
itakuwa ni kati ya Madini FC ya Arusha na JKT Ruvu ya Pwani watakaocheza
kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha wakati Kagera Sugar
itacheza Stand United ya Shinyanga Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mechi nyingine itakuwa ni kati ya
The Mighty Elephant ya Ruvuma na Ndanda FC ya Mtwara zitakazopambana
kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ilihali Azam na Mtibwa Sugar
watacheza Chamanzi –Mbagala – mchezo utakaofanyika saa 1.00 usiku.
Jumapili Februari 26, mwaka huu
timu ya Mbao FC itacheza na Toto Africans kwenye Uwanja wa CCM Kirumba
jijini Mwanza wakati Tanzania Prisons itacheza na Mbeya City zote za
Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
Machi 7, mwaka huu Young Africans SC itacheza na Kiluvya United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
No comments:
Post a Comment