![]() |
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje Marafiki wa Watoto wenye Saratani Tanzania, Janeth Manoni akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). ........................................................ |
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Asasi ya Marafiki wa Watoto wenye Saratani Tanzania wameandaa huduma ya upimaji wa saratani ya watoto bila malipo itakayotolewa Februari 18 mwaka huu katika viwanja vya Donbosco vilivyopo Upanga, Jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es
Salaam na Mkurugenzi wa Mambo ya Nje Marafiki wa Watoto wenye Saratani
Tanzania, Janeth Manoni alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu utoaji wa elimu juu ya kansa ya watoto.
Bi. Janeth amesema kuwa saratani
ya watoto ni janga kubwa ambalo wananchi wengi hawalifahamu kama
linaathiri kwa kiasi kikubwa hivyo lengo la Asasi hiyo ni kutoa elimu
juu ya ugonjwa huo.
”Utafiti uliofanywa mwaka
2015/2016 umeonyesha kuwa Tanzania tunategemea kuwa na watu 40,000 ambao
watakutwa na saratani kwa kila mwaka ambapo kati yao watoto ni 2500
hivyo, janga hili ni kubwa kwa watoto na linahitaji kupewa kipaumbele
ili kupunguza idadi yake”,alisema Bi. Janeth.
Ameongeza kuwa saratani za watoto
zikigundulika mapema zina uwezo wa kupona kwa asilimia 80 lakini tatizo
lilopo ni kucheleweshwa kufikishwa hospitali kwa sababu wazazi wengi
hawafahamu dalili za awali za kansa hiyo.
Kwa upande wake Muasisi wa Asasi
ya Saratani Tanzania Franklin Mtei, amesema kuwa wanaharakati wa sekta
ya afya wamejitolea kutoa elimu juu ya dalili za saratani ya watoto
kupitia mitandao ya kijamii pamoja na kutoa elimu siku hiyo ya upimaji.
Ametoa wito kwa wananchi
kujitokeza siku hiyo na kujijengea utamaduni wa kupima afya mara kwa
mara pamoja na kufanya mazoezi ili kuepuka kupata magonjwa mengine
yasiyoambukiza.
No comments:
Post a Comment