| Shughuli ya ubomoaji ikiendelea |
| Baadhi ya wananchi wakishuhudia shughuli ya ubomoaji ikiendelea. |
| Bi,Gaudesia Mathias moja kati ya wananchi wakielezea namna hali ilivyojitokeza. |
| Baadhi ya thamani za ndani zikiwa Nje kwenye zoezi hilo |
| Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akizungumza na wananchi ambao makazi yao yalikuwa yamebomolewa. PICHA NA JOEL MADUKA IMEANDALIWA NA www.madukaonline.blogspot.com
Jumla
ya nyumba sitini na nane (68 )zenye wakazi zaidi ya 100 katika Mtaa na
kata ya Bombambili Wilaya na Mkoa wa Geita zimebomolewa kwa madai kuwa
wananchi waliokuwa wakiishi kwenye makazi hayo wamevamia hifadhi ya
Mistu bila ya ridhaa ya wakala wa mistune nchini(TFS) huku kukiwa na
malalamiko kwa baadhi ya wananchi wenye uwezo wakiachwa katika Eneo hilo
bira kuvunjiwa.
Maduka
online imefika katika Eneo hilo majira ya saa nane Mchana na kushudia
tinga tinga likiendelea na ubomoaji huku wanachi wakiendelea kutoa
baadhi ya thamani nje ya nyumba hizo huku jeshi la polisi likiwa na
Mabomo ya machozi pamoja na Risasi za moto kwa lengo la kuimalisha
ulinzi wakati wa zaoezi hilo.
Wakizungumza
na Maduka online wananchi hao walisema kuwa pamoja na Serikali
kuwabomolea kwa kukaa hapo kimakosa hata hivyo mshangao unakuja kutokana
na kwamba wanaobomolewa ni wao wenye hali ya chini wale wenye uwezo
nyumba zao zimeachwa hali ambayo imepelekea kumwomba Rais John Magufuli
kuwasaidia walau makazi ya kuishi kutokana na ugumu wa maisha ndio
chanzo cha wao kuvamia maeneo ya hifadhi ya Mistu.
“Tuliishi
kwa miaka mingi sana na viwanja tuliuziwa na viongozi wa mitaa kwa
barua na tulianza ujenzi mara moja lakini leo wamekuja na kuanza kubomoa
kwa madai tumevamia Hifadhi ila kinachosikitisha kuna Nyumba za vigogo
zimebaki kwenye Eneo wanalosema ni Mstu hapa kuna uonevu Mkubwaa sana
Tunaomba Rais asikie Kilio chetu”alisema Aginesi John Mkazi wa mtaa huo.
“Mimi
ni mjane nilipoteza mme wangu tangu mwaka 2011 aliniachia watoto 5
nasomesha mimi ndiye baba Nyumba yangu wamebomoa na vitu vyangu viko nje
kama mnavyoona nitakwenda wapi nitalala wapi, nitakula wapi, mi sina
ndugu hapa Geita na wakati wansema Serikali ya Rais John Pombe Maguli ni
ya wanyonge lakini sisi tunazidi kukandamizwa kama mlivyoshudia alisika
akipiga Mayoe”Gaudesia Mathias.
Meneja
wa TFS Wilaya ya Geita Fredy Ndandika alisema opalesheni hiyo ilianza
tangu mwaka jana na wanachi walikuwa na taarifa za kuondoka na kupisha
hifadhi huku akikanusha taarifa za kwamba walivamiwa na kuanza kubomoa
na kuwata kuanza kufata sheria zilizowekwa na Mistu kwa kuzieshimu.
“Tulikuja
hapa tangu Mwaka jana na kuanza kutoa matangazo kwa wananchi waliovamia
Msitu wa Geita lakini waligoma kuondoka ndio maana leo tumeamua kuvunja
kwa kutumia nguvu na tataendelea kuwaondoa na kuvunja Nyumba zote za
watu waliovamia Hifadhi za Mistu”alisema Ndandika
Kwa
upande wake mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ambaye ni Mkuu wa
Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alikuwa msimamizi wa zoaezi
hilo alisema kuwa wakati maeneo hayo yanatolewa yeye akuwa kiongozi
Ndani ya Wilaya hiyo laki amesema kama wananchi waliuziwa maeneo hayo
kwa kudanganywa wapeleke vielelezo Ofisini kwake kuanzia siku ya
jumatatu na waliousika watachukuliwa hatua kali kwa kuwadanganya wenzao.
“Mimi
nafata maagizo yaliotolewa na Naibu Waziri wa Mazingira lakini kama
kuna wananchi wangu waliuziwa viwanja na Viongozi kwa kudanganywa
wavilete siku ya jumatatu Ofisini kwangu nitasimamia watarudishiwa fedha
zao na kuchukuliwa hatua kali kwa kuwaibia wenzao kwani huo ni wizi
kama wizi mwingine”alisema Kapufi.
Hivi
Karibuni wakati wa Ziara yake Mkoani Geita Naibu Waziri wa Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina alipata nafasi ya
kuzungumza na wananchi hao ambapo aliwaomba kuondoka kwa hiyari kwenye
hifadhi hiyo na kwamba wafate taratibu ambazo zimewekwa na serikali .
|
0 Comments