Waziri wa Nishati na
Madini, Prof. Sospeter Muhongo akisalimiana na baadhi ya Wahanga wa ajali ya
kufukiwa na kifusi katika mgodi wa RZ, Mkoani Geita. Prof. Muhongo alifika
mgodini hapo wakati wa ziara yake mkoani
humo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita
Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga (katikati) akimuongoza Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake kuelekea katika eneo la mgodi wa dhahabu
wa RZ.
Mkuu wa MKoa wa Geita
Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga akimwongoza Waziri wa Nishati na Madini, Prof.
Sospeter Muhongo katika eneo la mgodi ambapo wachimbaji wadogo 15 walifukiwa na
kifusi.
Waziri wa Nishati na
Madini Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake wakitoka eneo la mgodi wa RZ ambako
wachimbaji wadogo walifukiwa na kifusi.
Wachimbaji wadogo
wakimwonesha Waziri wa Nishati na Madini
Prof. Sospeter Muhongo na ujumbe wake namna walivyookolewa baada ya
kufukiwa na kifusi katika mgodi wa
dhahabu wa RZ, uliopo eneo la Nyarugusu mkoani Geita.
Kamishna Msaidizi wa
Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi akiwaongoza Waziri wa Nishati na Madini
Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Mstaafu Ezekiel Kyunga na
ujumbe wake kuelekea katika eneo la mgodi ambako wachimbaji 15 walifukiwa na
kifusi na kuokolewa wote wakiwa hai.
...............................................
Waziri wa Nishati na
Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekutana na Wahanga wa Ajali ya kufukiwa na
kifusi katika Mgodi wa Dhahabu wa RZ
uliopo katika Kijiji cha Mawemeru, Nyarugusu Mkoani Geita iliyotokea tarehe 26
Januari, 2017.
Aidha, Prof. Muhongo
amewataka Makamishna Wasaidizi wa Madini kote nchini kuchukua hatua za haraka
kusimamia mazoezi ya uokoaji pindi
zinapotokea ajali migodini pasipo kusubiri miongozo ya Waziri.
Pia amewaagiza
Makamishna hao kufanya ukaguzi katika migodi mikubwa na midogo katika maeneo
nayo na kuongeza kuwa, zoezi hilo la ukaguzi linatakiwa kufanywa haraka.
Pia amemtaka Kamishna
Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Viktoria Magharibi, kufuta leseni zote za
uchimbaji madini ambazo hazifanyi kazi.
Akizungumzia kuhusu
kuwaendeleza wachimbaji wadogo chini, Prof. Muhongo amesema kuwa, Sera na
mipango ya Serikali ni kuwandeleza
wachimbaji hao na kuhakikisha kuwa, wanatoka katika uchimbaji mdogo kwenda
uchimbaji wa Kati.
Katika hatua
nyingine, Prof. Muhongo ameitaka Migodi Mikubwa yote nchini kujisajili katika
Soko la Hisa la Dar es Salaam na kueleza kuwa, migodi hiyo imepewa wiki 6 iwe imejiandikisha katika soko hilo.
Pia Prof. Muhongo
amemshukuru Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, Mkoa wa
Geita, Viongozi wa Wizara, Wachimbaji na kampuni zote zilizoshiriki zoezi la
uokoaji na kufanikiwa kuokolewa kwa wachimbaji 15 waliofukiwa na kifusi.






0 Comments