Msemaji wa chama cha Maafisa Mawasilino
Serikalini (TAGCO) Bw. Abel Ngapemba (wa
pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la kufanya mazoezi, kupima afya,kuchangia damu,leo
jijini Dar es Salaam katika ulioshirikisha
Jukwaa la Wahariri (TEF) pamoja na Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam. Tamasha
hilo litafanyika siku ya Jumamosi katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja Kuotoka kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa, Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Theophil Makunga na Katibu wa Klabu ya
waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Siyovera Hussein.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi
Zamaradi Kawawa (wa kwanza kulia) akitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es
Salaam kujitokeza kwa wingi kushiriki katika Tamasha la Mazoezi ambalo litawapa
wananchi fursa ya kufanya mazoezi na
kupima afya bure kuitikia wito wa Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.Wengine
ni wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo.
Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa
Dar es Salaam Bw.Siyovera Hussein akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari
(hawapo pichani) leo Jijini Dar es
Salaam wakati wa mkutano uliolenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika
Tamasha linalolenga kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi . Kulia
ni Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Theophil Makunga
Mwenyekiti wa Jukwaa
la Wahariri (TEF) Bw. Theophil Makunga akizungumza wakati wa mkutano huo leo
Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa
waandishi wa habari kushiriki katika tamasha hilo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa na
Msemaji wa chama cha Maafisa Mawasilino Serikalini (TAGCO) Bw. Abel Ngapemba
Baadhi ya waandishi
wa habari wakifuatilia mkutano huo Leo Jijini Dar es Salaam.
(Picha na: Frank Mvungi - Maelezo)
No comments:
Post a Comment