Na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Umoja wa Kilimo cha mbogamboga,
matunda na nafaka umetoa wito kwa vijana kutumia fursa zilizopo kwenye
Sekta ya Kilimo na si kusubiri kuajiriwa.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Mwenyekiti wa Umoja huo Joseph Kunguru wakati akizungumza na
waandhishi wa habari kuhusu mradi kambi ya kilimo ulioanzishwa na Umoja
huo.
Mwenyekiti huyo alisema kuwa
wameandaa mradi huo kwa lengo la kuhamasisha vijana kuona kilimo ni
ajira na pia kilimo ni biashara.
“Tuna wanachama 74 ambao
wanatarajia kwenda kambini ambapo kati ya hao vijana 23 ni wahitimu wa
vyuo vikuu, watapatiwa mashamba, mbegu, vitendea kazi pamoja na chakula
katika muda watakao kuwa huko ili kuwafanya waweze kumudu katika
shughuli za kilimo” alisema Bwa. Kunguru.
Aidha, alisema kuwa umoja huo
unaunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na madawa ya kulevya
kwa kuwachukua vijana ambao wameshapata matibabu kujiunga na mradi huo
ili kuweza kuwafanya wasirudi tena vijiweni.
Akifafanua zaidi Bwa. Kunguru
alisema kuwa ili kuendesha umoja huo kiuchumi kila mwanachama kwenye
kila zao atachangia asilimia tano ya mapato kwenye umoja kama fidia ya
vifaa pamoja na mbegu walizopata kutoka kwenye umoja huo.
Mbali na hayo, umoja huo umepanga kuanzisha ligi ya mpira wa miguu itakayojulikana kama Kilimo Kapu
kwa lengo la kuhamasisha vijana kujiunga kwa pamoja kama vikundi ili
kuweza kuwa na kambi za maendeleo ili kuweza kujikwamua kiuchumi na
kuinua pato la taifa.
No comments:
Post a Comment