Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles
Mkumbo akionyesha baadhi ya kete za Heroin ambazo zilikamatwa hivi
karibuni kutokana na misako inayoenndelea mkoani hapa.
(Picha na Rashid
Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha).
.....................................................................................
Na Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Wiki
chache baada ya Jeshi la Polisi mkoani hapa kukamata gunia 58 za bhangi
ambazo ziliteketezwa kwa moto na kuharibu hekari 31 za mimea ya zao
hilo katika maeneo ya Kismiri Juu na Engalaon wilayani Arumeru, Jeshi
hilo limeendelea na misako dhidi ya wauzaji, watumiaji na wasafirishaji
wa dawa za kulevya na kufanikiwa kuwakata watuhumiwa 80 katika misako
iliyofanyika kwa muda wa siku 4 tu.
Akitoa
taarifa hiyo leo asubuhi ofisini kwake mbele ya waandishi wa habari,
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo
alisema kwamba misako hiyo imefanikisha kukamata jumla ya kete 167 za
madawa ya kulevya aina ya Heroin pia misokoto 3,845 ya Bhangi na mirungi
kilogramu 33.
“Katika
misako hiyo ambayo ilifanyika wilaya zote sita za mkoa huu, watuhumiwa
54 walipatikana kwenye tuhuma za Bhangi, 14 ni tuhuma za Heroin na 12 ni
wa tuhuma za mirungi.” Alisema Kamanda Mkumbo.
“watuhumiwa
40 ni wauzaji wa madawa hayo huku 13 ni wale ambao walikuwa
wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na Bhangi na mmoja alikuwa
anasafirisha, watuhumiwa 14 wa Heroin kosa lao kupatikana huku 12 makosa
yao ni kupatikana na mirungi na hivyo kufanya idadi yao kuwa 80 ambao
ni wanaume na wanawake”. Alifafanua Kamanda Mkumbo.
Kamanda
wa Polisi aliwashukuru wananchi wa mkoa huu kwa ushirikiano wa utoaji
wa taarifa za uhalifu na kuwaomba waendelee kufanya hivyo na kutoa onyo
kwa wale wachache wanaojihusisha na uhalifu wa namna hiyo waache mara
moja vinginevyo watakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
No comments:
Post a Comment