Baada ya timu sita (6) kutinga
hatua ya Sita Bora yaLigi Kuu ya Wanawake ya Shirilkisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) kufahamika,ratiba rasmi ya michuano hiyo, imetoka
na inaonyesha kuwa hatua hiyo ya kutafuta bingwa wa msimu, itaanza
Februari 18, mwaka huu.
Timu sita zilizofanikiwa kufika
hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya
Pwanina Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo
Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo,
kutakuwa na mechi mbili kila siku katika kituo kimoja kwa mujibu wa
kanuni. Kituo hicho ni Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es
Salaam ambako mchezo wa kwanza utaanza saa 8.00 mchana wakati mwingine
utaanza saa 10.00 jioni.
Ratiba inaonesha kwamba siku
ya Februari 18,mwaka huu kutakuwa na mchezo Kati ya JKT Queens na
Mlandizi saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na mchezo kati ya
Fair Play na Sisterz.
Februari 20, mwaka huu
kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na Panama saa 8.00 mchana
wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi na Fair Play.
Februari 22, mwaka huu
kutakuwa na mchezo kati ya Sisterz na Marsh Academy saa 8.00 mchana
wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na JKT Queens.
Februari 24, mwaka huu
kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na JKT Queens saa 8.00 mchana
wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Marsh Academy na
Mlandizi Queens.
Februari 26, mwaka huu
kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Sisters saa 8.00 mchana wakati saa
10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Marsh Academy.
Februari 28, mwaka huu
kutakuwa na mchezo kati ya Sisters na Mlandizi Queens saa 8.00 mchana
wakati saa 10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Panama na Fair Play.
Machi 2, mwaka huu kutakuwa na
mchezo kati ya Marsh Acedemyna Fair Play saa 8.00 mchana wakati saa
10.00 jioni kutakuwa na mchezo kati ya Mlandizi na Panama.
Machi 3, mwaka huu kutakuwa na mchezo mmoja tus aa 10.00 jioni ambako JKT Queens watamaliza na Sisterz.
No comments:
Post a Comment