IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE
Mbunge
wa Geita Mjini Constatine Kanyasu amesikitishwa kwa kitendo cha
wananchi waliokuwa wamejenga kwenye hifadhi ya misitu kubomolewa huku
wengine wakiachwa katika maeneo hayo na kuahidi kushughulikia ili haki
itendeke sawa na wale ambao hawajabomolewa.
Hayo
aliyasema kwenye mkutano wa hadhara ambao umefanyika kwenye mtaa wa
Mwatulole kata ya buhala hala wilaya na Mkoa wa Geita,wenye lengo la
kusikiliza na kutatua kero za wananchi katika jimbo ambalo analiongoza.
Mh
Kanyasu amesema kuwa amesikitishwa na hatua ya TFS kubomoa nyumba za
watu wengine huku wale wenye uwezo wakiachwa na kuendelea kukaa kwenye
maeneo hayo kutokana na hilo wameagiza watu wa TFS kuangalia kama wale
waliobomolewa pale yalikuwa ni maeneo yao na ninani ambaye aliwauzia.
“Naomba
Nikiri na mimi iliniuma sana lakini kwa sababu ni serikali na sikuwepo
na sijui kama walitumia sheria mimi naomba yeyote ambaye ni haki yake
ya msingi alete na mimi nitashughulikia”Alisema Kanyasu
Hata
hivyo Bi,Chausiku Lusetula ambaye ni miongoni mwa wanananchi
waliobomolewa makazi yao amemuomba Mbunge kuwasaidia ili wapate haki zao
za msingi na kwamba kwa sasa hawana makazi ya kuishi baada ya makazi
yao kubomolewa.
“Mheshimiwa
Mbunge sisi ni watu ambao tumekosa makazi kwa sasa hatujui ni wapi
tutaishi na chakusikitisha kwanini sisi tubomolewe na wengine waendelee
kukaa kwenye maeneo ambayo inasemekana ni hifadhi ya misitu kama ni
hivyo ni vyema haki itendeke kwa wote”Alisema Chausiku
Diwani
wa kata ya Buhala hala ,Mussa Kabese amewaambia wananchi kuwa mbunge wa
jimbo la Geita Mjini tayari amekwisha mwandikia Waziri mwenye dhamana
barua ambayo imemwomba matumizi ya pori la buhala hala kubadilishwa na
kuwekwa taasisi ambazo zitawasaidia wananchi ambao wapo kwenye mitaa ya
shinde na magogo kupata mahitaji ya msingi ikiwemo swala la elimu na
afya.
Hatua
hii imekuja ni baada ya takribani wiki mbili kumalizika ambapo wananchi
ambao wamejenga kwenye hifadhi ya misitu inayosimamiwa na wakala wa
misitu nchini TFS kubomolewa makazi yao.
|
0 Comments