
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Sightsavers Tanzania Gospert Katunzi akimkabidhi
Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo mashine ya uchunguzi wa uwoni baada
ya kufungua kambi ya uchunguzi wa macho katika kijiji cha Uroa Mkoa
Kusini Unguja. (kushoto) Mbunge wa Jimbo la Chwaka Bangwanji Mensuria
Mshamba ambae alifanikisha kambi hiyo.

Abdulrahaman
Abdalla wa Kitengo cha macho cha Mikunguni akimfanyia uchunguzi wa
macho mwanafunzi Hafsa Suleiman Ali katika kambi ya uchunguzi wa macho
Kijiji cha Uroa inayoendeshwa na Lions Club ya Dar es salam.

Mratibu
wa Lions Club ya Dar es salaam Mustasir Gulamhussein akimuhoji Bibi
Saumu Pandu Simai namna anavyoweza kuona baada ya kumpima na kumpatia
miwani kutoakana na matatizo aliyonayo.

Mbunge
wa Jimbo la Chwaka Bangwanji Mensuria Mshamba akizungumza na wananchi
wa Jimbo hilo waliofika kufanyiwa uchunguzi wa macho na kupatiwa dawa na
miwani kwa waliobanikia na matatizo ya uwoni.

Baadhi ya wananchi waliofika Skuli ya Uroa kuchunguzwa afya ya macho wakimsikiliza mbunge wao Bangwanji Mensuria Mshamba.

Picha
ya pamoja ya viongozi wa Lions Club ya Dar es salaam, wanaoendesha
kambi ya uchunguzi wa macho, wakiwa pamoja na Mbunge wa Jimbo la Chwaka
Bangwanji Mensuria Mshamba na Waziri Mahmoud Thabit Kombo.
Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.
0 Comments