Mwenyekiti
wa klabu ya Yanga ,Yusufu Manji akiwasili katika kituo cha Polisi Kati
jijini Dar es Salaam mara baada ya kuamua kujipeleka hapo yeye mwenyewe
kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65
aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho
Ijuma kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Mfanyabiashara
maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa
4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.
Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.
Manji
ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na
waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya
Ijumaa.
Amewasili leo na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi huku.
Manji amefika kituoni hapo akiwa na wanasheria wake 8
ambapo wanasheria 6 ni raia wa Tanzania na wanasheria wawili ni raia wa
Uingereza. Aidha, mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa wingi kituoni
hapo kumuunga mkono kiongozi wao.
Mbali na Manji, wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Pamoja na Fremaan Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, Iddi Azan.


0 Comments