Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya
Ujenzi Uchukuzi na Mwasiliano Bibi Elizabeth Tagolla (aliesimama) akifungua kikao
cha baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kinachofanyika
uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (kushoto) akimkaribisha Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi Elizabeth Tagolla kufungua kikao cha Baraza la wafanyakazi TEMESA kinachofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Wajumbe wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi
kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiimba kwa pamoja wimbo wa
wafanyakazi. Baraza hilo la siku moja linafanyikia uwanja wa Taifa jijini Dar
Es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Baraza la
wafanyakazi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakifuatilia mada mbali
mbali zinazo wasilishwa kwenye baraza hilo la siku moja linalofanyika uwanja wa
Taifa jijini Dar Es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Baraza la
wafanyakazi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiwa kwenye picha ya pamoja
na mgeni rasmi Bibi Elizabeth Tagolla (aliyeketi katikati). Baraza hilo la siku
moja linafanyika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu (kushoto)
akiagana na Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Bibi Elizabeth Tagolla (kulia) aliyekuwa mgeni rasmi katika kikao
cha baraza la wafanyakazi TEMESA kinachofanyika uwanja wa Taifa jijini Dar Es
Salaam.
Picha
zote na Alfred Mgweno – TEMESA







0 Comments