Mwenyekiti
wa Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango ambaye
pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, akitoa hotuba ya
ufunguzi wa mkutano huo kwa niaba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt.
Philip Mpango (Mb), Mjini Morogoro.
Mkurugenzi
wa Idara ya Huduma za Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa,
akitoa nen0 la shukrani baada ya hotuba iliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Bi. Dorothy Mwanyika, akifungua mkutano wa Baraza hilo kwa niaba ya
Waziri wa Fedha na Mipango wa Wizara hiyo, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Mjini
Morogoro.
Katibu
wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Cyprian Kuyava,
akizungumza wakati wa Mkutano wa 13 wa Baraza hilo, Mjini Morogoro.
Wajumbe
wa Mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakisikiliza
kwa makini maelezo ya mafanikio ya Mkutano wa Baraza hilo kwa mwaka 2015/2016
ambayo ni pamoja na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi, Mkutano uliofanyika Mjini
Morogoro.
Wajumbe
wa Mkutano wa 13 wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango wakiimba wimbo wa mshikamano daima,
mjini Morogoro.
Viongozi
waliokaa meza kuu, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Mkutano wa 13 wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakiimba wimbo wa mshikamano daima,
mjini Morogoro.
Mkurugenzi
wa Mipango Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Richard Mkumbo (aliyesimama)
akisalimiana na Viongozi waandamizi wa Wizara hiyo kabla ya kuanza kwa mkutano
wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango mjini Morogoro.
Meza
Kuu (Walioketi Mbele) wakiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na
Mipango, Bi. Dorothy Mwanyika, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa idara
na vitengo wa Wizara hiyo, mjini Morogoro.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi. Dorothy Mwanyika akitoka ukumbini
alipoongoza Mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara hiyo, Mkutano
unaofanyika mjini Morogoro.
(Picha
na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
....
Na
Benny Mwaipaja, WFM-Morogoro
Watumishi
wa Wizara ya Fedha na Mipango nchini wametakiwa kuendelea kuunga mkono juhudi za
Serikali za kuiletea nchi Maendeleo ya haraka kupitia falsafa ya uchumi wa
viwanda utakao iwezesha nchi kuwa ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa
kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kusimamia matumizi yake ipasavyo.
Rai
hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, katika Hotuba
iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Dorothy
Mwanyika, wakati akifungua mkutano wa 13 wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara
hiyo unaofanyika mjini Morogoro kwa siku mbili.
Bi.
Mwanyika amesema kuwa Mabaraza ya
wafanyakazi sehemu za kazi, yana malengo ya
kuongeza tija, ufanisi na ushirikishwaji wa wafanyakazi katika uongozi wa pamoja mahali pa kazi kama
agizo la Rais Na. 1 la mwaka 1970 likisomwa pamoja na miongozo mingine linavyo
elekeza.
Aidha
amewataka wajumbe wa Baraza hilo kukumbuka maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi
wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, kuhusu kusimamia ukusanyaji wa mapato na nidhamu ya matumizi ya Fedha
za Umma, ili kujenga uchumi wa Viwanda na kufikia maendeleo stahiki.
“Tuunge
mkono juhudi za Serikali kwa kutafsri maelekezo ya viongozi kwa vitendo ili
kuthibitisha msemo usemao Wizara ya Fedha na Mipango ndiyo moyo wa Serikali”
alisisitiza Bi. Mwanyika.
Pia
Bi. Mwanyika amewashukuru viongozi wa Wizara hiyo kwa kufanikisha mpango wa
Serikali wa kuhamia Dodoma ambapo katika awamu ya kwanza wafanyakazi 184
wameripoti mkoani humo licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo
ukosefu wa makazi. Hata hivyo amewataka
watumishi hao kushirikiana katika kutatua changamoto hizo kwa pamoja.
Kwa
upande wake Katibu wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara hiyo Bw. Cyprian Kuyava, amebainisha mafanikio
yaliyopatikana kutokana na maazimio
mbalimbali ya Mkutano uliopita wa mwaka
2015/2016 kuwa ni pamoja na kuboresha huduma kwa watumishi, kuboresha
mazingira ya kazi na kuongezeka kwa mshikamano miongoni mwa wafanyakazi licha
ya ufinyu wa Bajeti.
Naye
Mkurugenzi wa huduma za Sheria wa Wizara ya Fedha na Mipango Bi Susana Mkapa
amesema Watumishi wa Wizara hiyo wako tayari kuunga mkono juhudi za Serikali za
ukusanyaji wa mapato, kubana matumizi na hatua ya Serikali kuhamia Dodoma.
Mkutano
wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Fedha unafanyika kwa siku mbili kuanzia
Machi 27 hadi 28, 2017, huku ajenda kuu ikiwa kufanya mapitio ya utekelezaji wa
Bajeti ya Mwaka 2016/2017 na kujadili makadirio ya bajeti ya mwaka 2017/2018.
0 Comments