Random Posts

BODI YA WADHAMINI YA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) YAFANYA KIKAO CHAKE CHA KWANZA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

 Katibu wa Bodi ya Wadhamini  ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi akisoma taarifa ya Taasisi katika kikao cha kwanza cha Bodi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ambaye pia ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu Prof. William Mahalu.
 Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini  ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakifuatilia  taarifa ya Taasisi hiyo iliyokuwa  ikisomwa na Katibu ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Prof. Mohamed Janabi katika kikao cha kwanza cha Bodi  kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti  wa Bodi ya Wadhamini  ya Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambaye pia ni Daktari Bingwa wa upasuaji wa Magonjwa ya Moyo na mishipa ya damu Prof. William Mahalu akiongoza kikao cha kwanza cha bodi hiyo kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.

Picha na Anna Nkinda - JKCI

Post a Comment

0 Comments