Wana
Jogging wakifanya mazoezi
Wana-Jogging wakifanya mazoezi
Mwenyekiti wa Dar Jogging, Ramadhani Namkoveka akiwaongoza wenzake katika mbio
hizo.
Wana-Jogging wakipasha viungo kabla ya kuanza kukimbia 'mdogomdogo'.
Moja ya
manjonjo ya wana-jogging wakati wa kufanya mazoezi. Manjonjo hayo uwasaidia
kutokufikiria kuchoka.
Mwenyekiti wa Dar Jogging, Ramadhan Namkoveka akizungumza wakati wa Tamasha la
vikundi vya Jogging Temeke.
Wanachama wa
Umoja wa vilabu vya jogging (Uvijo) umeomba uongozi wa Chama Cha Kuogelea
nchini (TSA) kuandaa mavunzo yamchezo wa kuogelea kwa vijana chipukizi.
Ombi hilo
lilitolewa na wanachama wa umoja huo wakati wa tamasha kubwa la vikundi vya
jogging lililofanyika hivi karibuni kwenye uwanja wa Mwembe Yanga.
Katika
tamasha hilo ambalo lilianzia uwanja wa Taifa, wamia ya wanachama walisema kuwa
ni wakati wa wao kuanza kujifunza mchezo huo ili kuendeleza mazoezi kwa ajili
ya kuhimarisha afya zao.
Wanachama
hao walisema kuwa mchezo wa kuogelea ni mzuri kwa ajili ya mazoezi ya mwili
kwani uwezesha viungo vyote kutumika wakati wa mazoezi.
Mwenyekiti
wa Dar Jogging, Ramadhan Namkoveka ambaye pia ni katibu mkuu wa TSA alipokea
ombi hilo na kuahidi kulifisha kwa viongozi wenzake kwa akjili ya kutoewa
maamuzi.
Wakati huo huo; Uvijo imeanzisha mkakati wa
kuviinua kwa uchumi vikundi wanachama wake.
Mkoveka
alisema kuwa kuanzia sasa Uvijo ikitoa msaada wa fedha vilabu wanachama kwa
lengo la kuendesha miradi yao ya klabu, kukuza sekta ya michezo kwenye mazoezi
na vifaa na pamoja na kukuza upatikanaji wa ajira ndani ya vilabu rafiki vya
uvijo.
Hii ni mara
pili ndani ya umoja huu ambapo mwaka jana waliweza kuichangia klabu ya Dar
Jogging kiasi kama kilichochangwa mwaka
huu.
Vilabu
wanachama wa Uvijo ni Dar Jogging, Dovya
Jogging, Tupo Jogging, Barafu Jogging, Mzimuni Jogging, Tunajenga
Jogging, Wasafi Jogging na Temeke Family.
Tamasha hilo
lilifanikiwa kwa msaada wa Times FM Radio, Ndanda Spring water, pamoja na
huduma ya kwanza ikitolewa na G1 Security ambao walitoa madaktari pamoja na
Ambulance.




0 Comments