Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina
Mdeme akizungumza na wakazi wa Kata ya Nala alipowatembelea na kusikiliza maoni
na changamoto mbalimbali zilizopo katika kuanza kutekelaza radi wa ujenzi wa
Uwanja wa Michezo wa Kimataifa Dodoma.
Diwani wa Kata ya Nala Mhe. Brayceon Leonard
Eliah akiwasisitiza wakazi wa Kata yake kutoa ushirikiano kwa Serikali katika
kutekeleza mradi huu wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mkoa ya Uratibu
Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimatafa Dodoma Bw.Salum Mkuya akitoa mrejesho wa mambo yaliyofanywa na Kamati
yake kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme(Hayupo Pichani) katika
kuhakikisha Mradi huo unafanikiwa.
Afisa Mipango Miji Manispaa ya Dodoma Bw.
Clemence Msuva akieleza taratibu za tathimini ya eneo lililopo katika Kata ya
Nala utakapojengwa uwanja wa Michezo wa Kimataifa zitavyofanyika ili kuwezesha
mradi huo kuanza mapema.
Mmoja wa Mkazi wa kata ya Nala Stanley
Wilson akiuliza swali kwa Kamati Ndogo ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa
Uwanja wa Michezo wa Kimatafa kuhusu utekelzaji wa mradi huo na faida
watakazopata wakazi wa kata ya Nala na Dodoma kwa ujumla.
Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari
Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Evordy Kyando akiwahakikishia wakazi wa Kata ya Nala
kuwa Sheria na Taratibu zitafuatwa katika ulipaji wa fidia kwao.
Baadhi ya wakazi wa kata ya Nala wakimsikiliza
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme(Hayupo Pichani) alipowatembelea
na kusikiliza hoja mbalimbali juu ya mradi wa ujenzi wa wa Uwanja wa Michezo wa
Kimataifa unaotarajiwa kujengwa Mjini Dodoma.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
..................................................
Na
Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Mkuu
wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Christina Mdeme amewatahadharisha wakazi wa Kata ya
Nala watakaofanya aina yoyote ya udanganyifu katika ulipaji fidia kwao kwa
ajili ya mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa utaojengwa Mjini
Dodoma.
Ameyasema
hayo wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wa Kata ya Nala alipowatembelea na kusikiliza
hoja mbalimbali juu ya mradi wa ujenzi wa wa Uwanja wa Michezo wa Kimataifa
unaotarajiwa kujengwa Mjini Dodoma.
“Wewe
kama unajijua sio mkazi halali wa eneo unapopita mradi huu naomba ukafute jina
lako ila tukikubaini tutakuchukulia hatua kali za kisheria” alisisitiza Mhe.
Christina.
Mhe.
Christina Mdeme ameongeza kuwa Serikali haipo tayari kupoteza hela kwa ajili ya
kulipa watu wasiostahili katika mradi huo na kwamba kila anayehusika kulipwa fidia kihalali atalipwa.
Aidha
Mhe. Christina Mdeme amewahakikishia wakazi wa Kata ya Nala kuwa Serikali
haitamdhulumu mtu yoyote na atahakikisha kila anayepaswa kulipwa fidia analipwa
fidia anayostahili.
Pia
amewatahadharisha wakazi hao kutotumiwa na viongozi au vikundi vya watu kwa
manufaa ya kujipatia pesa zinazotokana na fidia za mradi huo kwa njia za
udanganyifu.
Kwa
upande wake Mwanasheria kutoka Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw.
Evordy Kyando amewaomba wakazi wa Kata ya Nala kuwa watulivu na kwamba Sheria
na Taratibu za ulipaji fidia zitafuatwa kikamilifu katika zoezi hilo.
Akitoa
maelezo ya kwa niaba ya Kamati ya Mkoa ya Uratibu Mradi wa ujenzi wa Uwanja wa
Michezo wa Kimatafa, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Bw.Salum Mkuya amewahikikishia
wakazi wa Kata ya Nala ushirikiano kutoka kwa Kamati yake ili kufanikisha mradi
huu wa kimataifa.
Akizungumza
kabla ya kufunga mkutano huo Diwani wa Kata ya Nala Mhe. Brayceon Leonard Eliah
amewaomba wakazi wa Kata yake kutoa ushirikiano kwa maafisa wa Serikali
watakaokuwa wanatathimini maeneo yao kwa ajili ya ulipaji wa fidia.









0 Comments