Na.Alex Sonna
Hatimaye zile kelele za mashabiki
wa Yanga kuhusu suala la kuwasajali wachezaji muhimu wa Simba ambao
mikataba yao ilikuwa inaelekea ukingoni ambao wameamua kukata mzizi wa
fitini kwa kuongeza mikataba mipya katika klabu hiyo inayoongoza msimamo
wa Ligi Kuu Tanzania bara
Mwenyekiti wa usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe amesema kuwa wachezaji hao Ibrahim Ajibu na Jonas Mkunde
wamekubali kusaini miktaba ya miaka miwili kila moja huku ikiwa na
vipengele ambavyo vinawaruhusu endapo watapata timu nje ya nchi
wataruhusiwa kwenda kusaka maisha mapya.
Kuongeza mikataba ya wachezaji hao
kumezima tetezi za kujiunga na watani zao Yanga ambao wapo katika
kipindi kigumu kwa sasa kutokana na Mwenyekiti wao Yusuf Manji kuwa
chini ya Ulinzi kwa tuhuma za kutumia Madawa ya kulevya na kusababisha
account zake kufungiwa na Serikali.
Pia ni habari nzuri kwa mashabiki
na wapenzi wa klabu hiyo ambao wana kiu ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu
bara ambao wameukosa kwa miaka mingi.

0 Comments