Kuna msemo unasema ukisema cha
nini,wenzako wanajiuliza watakipata Lini baada ya kutupiwa Virango na
Mabingwa watetezi ambaye alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Wana jangwani
Mholanzi Hans Van Der Pluijm hatimaye amejiunga na klabu ya Singida
United iliyopanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Msimu ujao.
Inasemekana aliyekamilisha suala
nzima la usajili wa Kocha huyu ni Mbunge wa Singida ambaye ni Waziri wa
Mambo ya Ndani ya nchi Mhe.Mwigulu Nchemba na pia nimshabiki wa kutupwa
wa klabu ya Yanga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati ya Usajili ya klabu
hiyo ambayo itakuwa inatumia uwanja Mkongwe wa Nafua uliopo Mjini
Singida.
Ikumbukwe kuwa Mh.Nchemba
alimrudisha Pluijm kwenye klabu ya Yanga baada ya kutangaza kuiacha timu
hiyo baada ya tetezi za kuwa nafasi yake inakuja kuchukuliwa na Kocha
wa sasa George Lwandamina na Mholanzi huyu alipandishwa cheo na kuwa
Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo hata hivyo hakudumu kwenye nafasi
hiyo ambapo alisitishwa Mkataba wake.
Pluijm amefundisha Yanga kwa awamu mbili tangu
mwaka 2014 alipoanza kwa kufanya kazi kwa nusu msimu, akimpokea Mholanzi
mwenzake, Ernie Brandts kabla ya kwenda Uarabuni.
Alikwenda Al Shoalah FC ya Saudi ya Arabia na nafasi yake
ikachukuliwa na Mbrazil, Marcio Maximo ambaye naye alifanya kazi kwa
nusu msimu kabla ya Pluijm kurejeshwa Januari mwaka jana.
Saudi Arabia ambako alikwenda na aliyekuwa Msaidizi wake, Yanga
SC, Charles Boniface Mkwasa – Pluijm aliondoka baada ya kutofautiana
na uongozi wa timu uliotaka kumsajilia wachezaji asiowataka.
Kabla ya kuhamishiwa kwenye Ukurugenzi wa Ufundi, Pluijm
aliiongoza Yanga katika jumla ya mechi 128, akishinda 80, sare 25 na
kufungwa 23.
Katika mechi 19 za nusu msimu mwaka 2014, alishinda 11, sare
sita na kufungwa mbili, wakati katika mechi 110 za tangu mwaka jana,
alishinda 69, sare 19 na kufungwa 21.
Msimu uliopita ulikuwa mzuri zaidi kwake, akibeba mataji yote
matatu, Ngao ya Jamii, Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC).
Pluijm pia aliiwezesha Yanga kufika hatua ya makundi ya
michuano ya Afrika (Kombe la Shirikisho) kwa mara ya kwanza tangu mwaka
1998 na mara ya pili kihistoria. Yanga ilifika hatua ya makundi ya Kombe
la Shirikisho mwaka huu baada ya mwaka 1998 kufika hatua ya makundi ya
Ligi ya Mabingwa.
Na kwa mafanikio hayo, haikuwa ajabu Pluijm akishinda tuzo ya
kocha bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mwishoni mwa msimu
uliopita.
Mapema wiki hii, Singida United ilimsajili kiungo Tafadzwa
Kutinyu kutoka Chicken Inn Fc ya Zimbabwe kwa mkataba wa miaka miwili.
Singida United imerejea Ligi Kuu msimu huu baada ya msoto wa zaidi ya miaka 15 tangu ishuke Daraja.

0 Comments