Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama, Balozi Adadi
Rajabu (wakwanza kushoto), akiongozana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada
ya kukagua Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Wa kwanza kulia ni Kamishna Jenerali wa
jeshi hilo, Thobias Andengenye.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya,
akijibu baadhi ya hoja zilizoelekezwa na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama
(hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea mradi wa ujenzi ofisi za
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Ziara hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Kamishna Jenerali wa jeshi hilo, Thobias Andengenye.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye akitoa taarifa ya
mradi wa ujenzi wa ofisi za jeshi hilo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama(hawapo pichani), wakati wajumbe hao walipotembelea
mradi huo leo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Balozi Adadi Rjabu na anayefuatia ni Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahaya.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mjumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Mambo ya Nje ya Ulinzi na Usalama,Kapteni Mstaafu George Mkuchika, akichangia
hoja wakati wa ziara ya kamati hiyo kukagua ujenzi wa ofisi za Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji, jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI




0 Comments