Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu ambaye pia alikuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii katika serikali ya awamu ya nne, ameguswa
na ishu ya kuvamiwa wa kituo cha Clouds Media pamoja na kitendo cha
aliyekuwa waziri wa habari Nape kutishiwa bastola ili asiongee na
waandishi wa habari muda mchache baada ya kupigwa chini kwenye baraza la
mawaziri na nafasi yake kuchukuliwa na Harrison Mwakyembe.
Wabunge wengi wa CCM walikuwa kimya dhidi ya sakata hilo ambapo
Ijumaa hii, Nyalandu ametaka matukio hayo kwenda kujadiliwa bungeni.
Kupitia twitter mbunge huyo alitweet,”IMESIKITISHA sana kuona
AFISA akimtishia silaha Waziri Mstaafu Nape.Kitendo hicho ni kinyume na
maadili ya TAIFA letu na kimedhalilisha NCHI,”
Aliongeza, “Kupitia BUNGE, nitaiomba SERIKALI ichukue HATUA
za kinidhamu na kisheria DHIDI ya AFISA aliyemtishia Mh NAPE kwa
SILAHA.Kitendo HAKIKUBALIKI,”
Katika sakata la RC Makonda kuvamia kituo cha Clouds Media alitweet,
“Katika kutekeleza wajibu wake KIKATIBA, BUNGE ni sharti lijadili na
kutoa AZIMIO kuhusu kilichojiri CLOUDS FM, na UHURU wa VYOMBO vya
HABARI,”
Pia kitendo hicho kimeweza kupingwa na mashirika mbalimbali habari nchini.

0 Comments