Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma , Jaji Mstaafu
Harold Nsekela wa kwanza kushoto akiwaongoza Makamishna wapya wa
Uhamiaji kuapa kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma baada
ya Makamishna hao wapya kuvalishwa vyeo vipya katika hafla
iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Dodoma.
Kamishna mpya wa Uhamiaji Divisheni ya Sheria Hannerole Morgan
Manyanga akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji
Dr. Anna Peter Makakala katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa
Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo
imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja
Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi
Hassan Simba Yahaya.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala ,akimvisha
cheo kipya Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha, Edward Peter
Chogero katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa
Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Anayeshuhudia ni Naibu
Kamishna wa Uhamiaji Chrispin Ngonyani. Tukio hili linehudhuriwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest
Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba
Yahaya.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira akitoa maelekezo kwa Makamishna wapya wa Uhamiaji
wakati wa hafla ya kuvikwa Vyeo Vipya iliyofanyika leo katika ukumbi
wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Makamishna wapya wa Uhamiaji wakisaini Fomu za Maadili ya
Viongozi wa Umma baada ya Makamishna hao kula kiapo cha Maadili ya
Viongozi wa Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo katika
ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali
Projest Rwegasira aliyeketi katikati akishuhudia Makamishna wapya wa
Uhamiaji wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma baada
ya kuvishwa vyeo vipya katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa
Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kulia ni Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya na kushoto ni
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala wote wakishuhudia
tukio hilo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali
Projest Rwegasira akizungumza jambo na Makamishna wapya wa Uhamiaji
baada ya kumalizika shughuli ya kuapishwa Makamishna hao leo katika
viwanja vya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.







0 Comments