Wanawake wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA)
wakiungana na mamia ya wanawake wengine duniani, kusherehekea Siku ya
Wanawake Duniani, iliyofanyika kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini
Dar es Salaam.
Siku ya Wanawake Duniani iliadhimishwa jana kwenye viwanja vya
Mwem be Yanga Jijini Dar es Salaam, ambapo wanawake kutoka Ofisi za
serikali na binafsi waliungana na wenzao kusherehekea siku hiyo muhimu.
Pichani ni wanawake kutoka Idara mbalimbali za Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Tanzania (TAA) wakifurahia siku hiyo.
Wanawake kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA),
wakiserebuka kwenye viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam,
wakiifurahia siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa jana, ambapo mgeni
rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaviva aliyemwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.
Wanawake wakiwa kwenye furaha wakiadhimisha Siku ya Wanawake
Duniani, iliyoadhimishwa jana katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar
es Salaam, ikiwa na kauli mbiu ya Tanzania ya Viwanda; Wanawake ni
Msingi wa Mabadiliko ya Kiuchumi.




0 Comments