Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea kesho
Jumamosi vinara wa ligi hiyo Simba inatarajiwa kuialika Mbeya City
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ukiacha
mchezo huo, michezo mingine ya kesho Jumamosi Machi 4, mwaka huu
itakuwa ni kati ya Toto Africans na Mbao FC kwenye Uwanja wa CCM
Kirumba, jijini Mwanza huku Kagera Sugar ikiikaribisha Majimaji ya
Songea kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
Azam
FC pia itacheza Jumamosi Machi 4, mwaka huu na Stand United ya
Shinyanga kwenye Uwanja wa Chamazi. Mchezo huo utaanza saa 1.00 jioni
wakati mechi nyingine zitaanza saa 10.00 jioni.
Jumapili
Machi 5, mwaka huu Mtibwa Sugar itaialika Young Africans kwenye uwanja
huo katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mchezo
mwingine wa Ligi Kuu ya Vodacom utachezwa Uwanja wa Uhuru ambako
African Lyon itaialika Mwadui ya Shinyanga wakati Ndanda FC itakuwa
mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona siku ya
Jumatatu Machi 6, mwaka huu.
..…………………………………………………………………………........................
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

0 Comments