Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Balozi wa Kupinga mauaji ya Tembo nchini Tanzania , Amon Mkoga, (katikati) akionesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya vipeperushi vya Dovu Marathon Dar es Salaam leo, kulia ni Meneja wa usalama kazini kutoka Kampuni ya Mafuta (PUMA) Boniphace Menchi, na Ofisa Masoko Hanson Heddi.
Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Balozi wa Kupinga mauaji ya Tembo nchini Tanzania , Amon Mkoga, (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo, kulia ni Meneja wa usalama kazini kutoka Kampuni ya Mafuta (PUMA) Boniphace Menchi, na Ofisa Masoko Hanson Heddi.
Meneja wa usalama kazini kutoka Kampuni ya Mafuta (PUMA) Boniphace Menchi akijibu mswali kwa waandishi wa habari.
Meneja Masoko wa Red Bull
Bw.Hanson Heddi akielezea akifafanua.
Je, itakuwaje kama tembo
wote nchini Tanzania watakwisha na kubaki tembo mmoja tu? Utafanyaje?
Utajisikiaje urithi wetu huu wa kustaajabisha ukipotea katika kizazi chetu?
Ndo maana Chief
Promotions ,kwa udhamini wa Puma Energy,D.T Dobie,Songas,EY,Red
Bull,Sayona,Colosseum Hotel ingependa ingependa kuutaarifu umma katika kuanzimisha
siku ya Wanyamapori Duniani Chief Promotions imeandaa mbio za Ndovu Marathon.
Mbio hizi zenye lengo la
kuongeza ufahamu na kuielimisha jamii kuhusu tatizo sugu la ujangili
linaloikabili Tanzania .Mbio hizi zinatarajiwa kuongeza mwamko kwa taasisi za
kiraia katika kulinda tembo na wanyama wengine.
Tanzania imepoteza asilimia 60 ya tembo wake katika miaka sita iliyopita zaidi
kutokana na ujangili kwa ajili ya pembe za ndovu. Wanaonufaika zaidi na pembe
za ndovu ni baadhi ya wafanyabiashara haramu wa nchini China na katika nchi
nyingine zenye watumiaji wa bidhaa zitokanazo na pembe za ndovu huku Tanzania
ikibaki kuwa muathirika wa tatizo hili.
“Watalii wengi wanaokuja nchini hupendelea zaidi kuwaona Tembo, na utalii
unachangia asilimia 12 ya pato letu la taifa (GDP)”, alisema Amon Mkoga ambaye
ni mratibu na Balozi wa Kupinga mauaji ya Tembo Tanzania. “Tembo wetu ni
utajiri mkubwa kwa nchi yetu katika njia mbalimbali na serikali yetu
imedhamiria kukomesha uhalifu huu. Hata hivyo hatuwezi kufanya jambo hili peke
yetu, tunahitaji kupata msaada wa wananchi wote katika jitihada zetu katika
kukomesha wizi huu wa urithi wa taifa letu”.
Katika utafiti wa hivi karibuni uliohusisha zaidi ya Watanzania 2,000 waishio
vijijini na mijini, zaidi ya asilimia 79 walioshiriki walisema kuwa
watasikitika endapo tembo watatoweka Tanzania na zaidi ya asilimia 73 walisema
wanaamini kuwa tembo ni utambulisho na urithi wa taifa.
Kauli mbiu ya mwaka huu
ya Siku ya Wanyamapori Duniani ni-Tusikilize Sauti za Vijana kwa kuwa mustakabali
wa baadae wa Uhifadhi wa wanyamapori ,mimea na mazingira upo mikoni mwao.




0 Comments