Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara ambao umefanyika katika kata ya Nyankumbu mmoja kati ya wananchi, Bi,Angelina Richard amemwambia mbunge wa
Geita Mjini ,Constatine Kanyasu kuwa tatizo la maji limekuwa ni tatizo
kubwa hususani kwa wakina mama hali ambayo imekuwa ikitishia kuvunjika
kwa miji yao.
“Mheshimiwa
Mbunge kiukweli sisi wakina mama tumekuwa tukiingia kwenye malumbano na
familia zetu sababu kubwa ni kutokupatikana kwa maji tunakuomba kama
mwakilishi wetu utusaidie”Alisema Bi Angelina.
Kutokana
na Ombi hilo ,Mbunge wa jimbo la Geita Mjini Constatine Kanyasu,alisema
kuwa wamepata Bilioni mia moja kutoka serikali ya India ambazo
zimekopwa na serikali ili kusaidia upatikanaji wa maji katika maeneo
ambayo yamekuwa na changamoto.
“Mkandarasi
anatarajia kuanza kazi mwezi wa saba kwa kuakikisha anasambaza maji
kwenye maeneo ambayo yameonekana kuwa na changamoto kubwa ya maji kwenye
halmashauri ya mji wa Geita kwa hiyo niwahakikishie wananchi kuwa swala
hili tunashughulika nalo na tutaakikisha changamoto hii
tunaimaliza”Alisema Kanyasu
Aidha kwenye mkutano huo,meneja ufundi wa Gewasa,Isaac Mgeni ,akisema kuwa tatizo la kukatika kwa maji linatokana na matengenezo ya miundo mbinu ambayo imekuwa ikitumika kutibia maji pamoja na kukatika kwa umeme kuwa kwenye matengenezo lakini hata hivyo bado wapo kwenye jitihada za kukomesha kero hiyo.
Diwani wa Kata ya Nyankumbu Michael Kapaya amewataka wananchi hao kuwa na subira kwani serikali imejipanga kutatua changamoto zinazo wazunguka hususani za miundo mbinu.
0 Comments