Eng.
Athu Chulla akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kulia), mara baada ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania
(TBA), katika eneo la Magomeni jijini Dar es Salaam. Pembeni kwa Naibu
Waziri ni Mratibu wa Ujenzi wa nyumba hizo, Arch. Christina Shayo.
Mratibu
wa Ujenzi wa nyumba zinazojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA),
Arch. Christina Shayo (wa kwanza kushoto), akifafanua jambo kwa Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani, mara
baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa nyumba katika eneo la Magomeni
jijini Dar es Salaam.
Muonekano
wa moja ya nyumba za wananchi zinazojengwa na Wakala wa Majengo
Tanzania (TBA) katika eneo la Magomeni ikiwa katika hatua ya msingi,
Nyumba hizo zinatarajiwa kuhudumia kaya 656 zitakapokamilia Septemba
mwaka huu.
Mafundi
wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakiendelea na ujenzi wa nyumba za
wananchi katika eneo la Magomeni. Nyumba hizo zinatarajiwa kuhudumia
kaya 656 zitakapokamilia Septemba mwaka huu.
Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment