“Tumedhamiria kujenga
Tanzania ya viwanda, tunawakaribisha wawekezaji kutoa Italia ili waje kuwekeza
kwenye viwanda vya usindikaji mazao ya mifugo pamoja na uvuvi kwa sababu
tunatambua kuwa ninyi mmebobea katika eneo hilo,” alisema.
Ametoa kauli hiyo jana
jioni (Jumanne, Februari 28, 2017) alipokutana na Balozi wa Italia nchini
Tanzania, Bw. Roberto Mengoni kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es
Salaam.
“Serikali ya awamu ya
tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda ili kuongeza ajira na kuondoa
umaskini miongoni mwa wananchi wake. Tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye maeneo
mbalimbali,” alisema Waziri Mkuu.
Kwa upande wake, Balozi Mengoni alimweleza Waziri Mkuu kwamba
katika muda wa miezi nane ambayo ameishi hapa nchini, amebaini kuwa Tanzania ni
nchi yenye fursa nyingi za kiuchumi. “Ni soko kubwa ambalo halijaguswa
(untapped market) hasa kwenye masuala ya viwanda na uwekezaji.
Hata hivyo, Balozi
huyo alikiri kwamba bado wananchi wengi wa Italia wanahitaji kupatiwa elimu
zaidi juu ya fursa zilizopo hapa nchini. “Hadi leo kuna Waitaliano ambao
hawajui kuwa Mlima Kilimanjaro uko Tanzania. Wengi wanajua uko Kenya, kwa hiyo
elimu zaidi inahitajika katika suala zima la kutangaza utalii wa Tanzania,”
alisema.
Alisema tangu afike
nchini, wawekezaji kutoka Italia wameonesha nia ya kuwekeza kwenye nishati
jadidifu, kiwanda cha kutengeneza nguo za michezo (sports wear) na kwamba
wafanyabiashara wengine zaidi wanatarajia kuja hapa nchini.
Ili kutoa uelewa mpana
kwa wafanyabiashara na raia wa Italia, ubalozi kwa kushirikiana na Kituo cha
Uwekezaji Tanzania (TIC) tumeandaa mkutano mkubwa kuhusu biashara na uwekezaji
utakaotoa maelezo kuhusu fursa zilizopo Tanzania katika nyanja mbalimbali.
“Mkutano huu
utakaofanyika Mei 6, mwaka huu, utawalenga zaidi wafanyabiashara na utajikita
kwenye maeneo makuu sita ambayo ni viwanda vya usindikaji, viwanda vya nguo
(textiles), ngozi na mazao yake, miundombinu, nishati na utalii,” alisema.
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amekutana na Balozi wa Japan hapa
nchini, Bw. Masaharu Yoshida ambapo katika mazungumzo yao wamejadiliana mambo
mbalimbali yakiweo ya miundombinu, elimu na nishati.
No comments:
Post a Comment