Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuweka jiwe la
msingi la ujenzi wa barabara za juu (interchange), katika makutano ya
Ubungo tarehe 20 Machi, 2017.
Aidha Rais wa Benki ya Dunia
Mheshimiwa Dkt. Jim Yong Kim anatarajiwa kushiriki katika sherehe hiyo
ya uwekaji wa jiwe la msingi la interchange ya Ubungo.
Mradi wa ujenzi wa barabara za
juu katika makutano ya Ubungo ambao utagharimu takribani shilingi
bilioni 188.71 una lengo la kupunguza msongamano wa magari katika
barabara za Morogoro, Nelson Mandela na Sam Nujoma.
Mradi huu ni sehemu ya mradi wa
uboreshaji usafiri Jijini Dar es Salaam yaani (Dar es salaam Urban
Transport Improvement Project), utakaogharimiwa kwa mkopo kutoka Benki
ya Dunia na mchango wa Serikali ya Tanzania ambao utahusisha pia awamu
ya tatu na ya nne ya ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka
(Bus Rapid Transit- BRT), katika barabara ya Nyerere kutoka katikati ya
jiji la Dar es Salaam hadi Gongo la mboto na barabara ya Bagamoyo kutoka
katikati ya jiji hadi Tegeta.

0 Comments