
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini
kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ilulu Mkoani
Lindi. Wengine katika picha ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey
Zambi(Wakwanza kushoto), Waziri wa Maji Mhandisi Gerson Lwenge,
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Lindi Mzee Ally Mtopa pamoja na Mbunge mteule
Mama Salma Kikwete.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia
wananchi katika Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi kuhusu masula mbalimbali ya
mkoa huo pamoja na Taifa kwa ujumla.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga
mkono kuwaaga wananchi wa Lindi waliofika katika uwanja wa Ilulu
kumsikiliza mara baada ya kumaliza kuwahutubia uwanjani hapo.
PICHA NA IKULU
0 Comments