Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika
ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya
kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na
kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu
makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo
zisisafirishwe mahali popote.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na
kutoa maagizo mbalimbali kuhusu makontena 20 (yanayoonekana nyuma) yenye mchanga wa madiniuliokuwa usafirishwe
kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote.
Makontena
20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya
ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye maelezo kuhusu
makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini na Wafanyabiashara wakubwa kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari wanayoyachanganya na bidhaa zilizochakaa.
Moja
ya kontena likiwa lina gari ndani yake aina ya Range Rover ambapo muagizaji
alidai kuwa anaagiza mitumba lakini kumbe ndani yake anakuwa ameficha magari ya
kifahari.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo.
PICHA NA IKULU













0 Comments