Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Edwin Ngonyani akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati
wa maadhimisho ya siku ya hali ya hewa duniani mapema hii leo jijini Dar es
Salaam, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) Dkt.
Agnes Kijazi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi
akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho
ya siku ya hali ya hewa duniani mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kulia ni
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani.
Waandishi
wa habari wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania (TMA) Dkt. Agnes Kijazi (hayupo pichani) habari wakati wa maadhimisho
ya siku ya hali ya hewa duniani mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha
zote na Eliphace Marwa - Maelezo
...............................
Na: Frank Shija – MAELEZO.
WATANZANIA washauriwa kutembelea Vituo vya hali ya
hewa nchini ili kuona shughuli zitolewazo na Mamalaka ya Hali ya Hewa ikiwa ni muendelezo wa kujifunza na kuongeza
uelewa juu ya masuala ya hali ya hewa.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhandisi
Edwin Ngonyani wakati akitoa taarifa kuhusu maadhimisho ya siku ya Hali ya Hewa
duniani ambayo inafikia kilele chake leo tarehe 23 Machi.
“Katika kuadhimisha siku hii ya hali ya hewa dunia
ninatoa wito kwa wananchi kutembelea katika vituo vya hali ya hewa vilivyopo
katika maeneo mengi ya nchi ili waweze kujifunza zaidi juu ya hali ya hewa na
kuongeza uelewa hasa katika elimu juu ya mawingu,” alisema Mhandisi Ngonyani.
Aliongeza kuwa katika kuadhimisha siku hiyo mwaka
huu yamejikita katika kuongeza ulewa kwa
wananchi kuhusu elimu juu ya Mawingu ambapo kauli mbiu yake ni, “Tuyaelewe
Mawingu na Umuhimu Wake.”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya
Hali ya Hewa(TMA), Dkt. Agness Kijazi amesema kuwa wananchi ni muhimu kujenga
mazoea ya kufuatilia taarifa za hali ya hewa kwani ni muhimu katika shughuli za
maendeleo.
Alisema maadhimisho ya mwaka huu yamepewa msukumo
katika kuongeza uelewa wa wananchi kuhusu sayansi ya Mawingu na mchango wake
katika mzunguko wa maji kati ya nchi kavu, hali ya hewa ya muda mfupi na mrefu.
Maadhimisho hayo ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani
uadhimishwa tarehe 23 machi kila mwaka yakiusisha nchi 191 ambazo ni wanachama wa Shirika la Hali ya
Hewa Duniani ikiwa ni moja kukumbuka kuanzishwa kwa Shirika hilo mnamo mwaka
1950.



0 Comments