Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda pamoja na Mkuu Wilaya
ya Temeke, Felix Lyaniva wakikata utepe kuashilia kukabidhiwa barabara
ya Kusasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini
Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza katika
uzinduzi wa wa akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege
yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza katika
uzinduzi wa kukabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye
urefu wa Kilomita moja leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa na Mkuu wa
Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva na watendaji wakitembelea barabara
Kusasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja leo jijini
Dar es Salaam.
..........................
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul
Makonda amesema jiji la Dar es Salaam linatakiwa kubadilika katika
kufikia viwango vya majiji ya kimataifa. Makonda ameyasema hayo leo
wakati akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye
urefu wa Kilomita moja, amesema barabara hiyo ndio kiungo kikubwa kwa
upande wa bandari.
Mkuu
wa Mkoa ametoa onyo kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao
hapa jijini chini ya viwango ya kuwa kuanzia sasa kampuni hizo pale
zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi
na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini kwa miaka
mitatu.
"Wananchi
wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara,
wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama
hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi sita
haijapita" amesema Makonda .
Amesema
barabara hiyo imejengwa na kampuni ya kizalendo ya Grant Tech Company
ya jijini Dar es Salaam na maombi ya barabara ni miezi miwili iliyopita
lakini imekamilika kwa muda mwafaka .
Makonda
amesema miundombinu ya barabara ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi
kwa taifa lolote lile. Makonda ameelekeza manispaa zote zisimamie vyema
fedha za barabara ili kupunguza adha za usafiri kwa wananchi wa Dar es
salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye mashimo zinazoleta
hitilafu hata kwa vyombo vyao vya usafiri.
Makonda
amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga
Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ni ndoto ya Rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia
Tanzania ya viwanda inaendelea kutimia.
Mkandarasi
huyo (Grant tech), Masito Mwasingo amesema kuwa wamefanya ujenzi kwa
muda mwafaka kutokana umuhimu na kuunga kuunga mkono utendeji kazi wa
serikali ya mkoa wa Dar es salaam.




0 Comments