Na John Luhende Mwambawahabari
Wito umetolewa kwa wazazi na walezi wenye Watoto wenye mahitaji maalumu kutowaficha ndani na kuwa acha bila msaada watoto wenye matatizo ya Usonji na kutambua kuwa ni zawadi kutoka kwa Mungu na wanastahili kupatiwa Elimu sawa na watoto wengine .
Akizungumza na waandishi wa habari kwaniaba ya mkuu wa shule hiyo mwalimu mwalimu mkuu msaidizi wa shule ya Wasichana Almuntazir (AMSEN) Bi Joan Soka ameitaka jaamii kuto watenga watoto hao kwa kuwa nawao wanahakisawa na watoto wengine na wana haki ya kupatiwa Elimu .
Aidha Soka amesema matembezi hayo yata saidia kuhamasisha jamii kuwa na uelewa kuhusu watoto hao wenye matatizo ya usonji uliko ilivyo sasa ambapo wato wengi wenye matatizo jamii haiwajali.
Pamoja na hayo Amesema kuwa tangu kuanzishwa kwa shule hiyo mwaka 2013 watoto wengi walio soma shule hiyo wamesaidiwa kupata elimu na ambayo imeweza kuwa saidi a katika maisha yao na baadhi yao wameajiriwa kufanya kazi katika taasisi na makampuni kufanya kazi mbalimbali kulingana na halizao na wame weza kujipatia kipato.
Matembezi hayo yanafanyika kwa mara ya pili na yatafanyika siku ya Usonji Duniani (AUTISM DAY) tarehe 2/ April 2017 saa 2: 30 yata anzia shule ya Shule ya Wavulana Almuntazir na kuishia katika Shule ya wasicha Almuntazil ,,,,,,Kauli mbiu mwaka huu ni ‘’ Tuwalinde na Tuwapende,,

0 Comments