Baadhi ya wazazi ambao watoto wao wamekwenda
nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya magonjwa ya moyo wakifuatilia kwa karibu
mkutano wa waandishi wa Habarai uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma ya Uuguzi kutoka
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Robert Mallya akiwaongoza watoto
wanaokweda kutibiwa magonjwa ya moyo
nchini Israel kuingia kwenye gari kwa ajili ya kwenda uwanja wa ndege kuanza
safari ya kuelekea nchini humo. Serikali kupitia JKCI kwa kushirikiana na Serikali ya Israel
kupitia Taasisi ya Save Child Heart imewapeleka watoto nane (8) nchini humo kwa
ajili ya matibabu ya moyo.
Wataalamu
wa Magonjwa ya Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) , ndugu na
watoto wanaokwenda kutibiwa nchini Israel wakiwa katika picha ya pamoja kabla
ya kuanza kwa safari ya watoto hao ya kuelekea nchini humo kwa ajili ya
matibabu ya moyo.
Mkutano
na waandishi wa Habari kuhusu watoto nane
wanaokwenda kutibiwa magonjwa ya moyo
nchini Israel ukiendelea leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya
Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) . Serikali kupitia JKCI kwa kushirikiana na Serikali ya Israel
kupitia Taasisi ya Save Child Heart imewapeleka watoto nane (8) nchini Israel
kwa ajili ya matibabu ya moyo.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji wa Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
(JKCI) Godwin Sharau akiongea na waandishi wa habari kuhusu watoto nane
wanaokwenda nchini Israel kwa ajili ya
matibabu ya moyo. Hili ni kundi la nne la watoto kwenda kutibiwa nchini humo
tangu mwaka 2015 ambapo JKCI ilianza ushirikiano na Taasisi ya Save Child Heart ya kuwapeleka wagonjwa nchini Israel hadi
sasa watoto 40 wameshatibiwa na wanaendelea vizuri. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
wa Huduma ya Uuguzi Robert Mallya.







0 Comments