Random Posts

TAMASHA LA PASAKA KUFANYIKA UWANJA WA UHURU



Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Tamasha kubwa la muziki wa injili linalofahamika kama Tamasha la Pasaka sasa kufanyika katika uwanja wa Uhuru april 16 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mratibu wa Tamasha hilo Alex Msama amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na sasa uwanaj wa uhuru ndio sehemu maalum ya kuanzia Tamasha hilo jijini Dar es Salaam.

“Malengo ya tamasha la pasaka ni yaleyale ni kuliombea taifa na kumuombea Rais wan chi Dkt John Pombe Magufuli  hili aendelee kutawala kwa amani katika taifa hili” amesema

Ametaja kuwa tamasha hilo kwa sasa litatembea katika mikoa kumi na kufanya uzinduzi wa albamu mbili

Post a Comment

0 Comments